Bia ya kimataifa ya Heineken leo imetangaza mpango wa ziara ya Kombe la Mabingwa wa Ligi ya Ulaya (UEFA) 2012 katika Afrika Mashariki kwa udhamini wa Heinken. Heinken inaleta kombe hilo muhimu kwenye soka ya klabu kwa wateja wake pamoja na mashabiki wa mpira wa miguu nchini Tanzania.
Heineken imekuwa na uhusiano na Mabingwa wa Ligi ya Ulaya tangu msimu wa mwaka 2005/06 na itabakia kuwa moja ya wadhamini wakuu kwa ligi hiyo hadi msimu wa 2014/15. Hii inakuwa ni ziara ya sita ya Komnbe hilo kufanywa na Heineken lakini ikiwa ni ya kwanza kufanyika sehemu mbalimbali duniani. Ziara ya kombe hilo kwa udhamini wa Heineken ilishafanyika Asia mwaka 2011, Marekani mwaka 2010, Afrika mwaka 2009, Amerika Kusini mwaka 2008 na barani Asia mwaka 2007.
Ziara hii ya Kombe la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kupitia udhamini wa Heinken itaanza safari yake katika nchi za Afrika Mashariki ikianzia Nairobi hadi Dar es Salaam kupitia Mombasa na baadae kurudi Nairobi. Baada ya hapo safari itaelekea Shanghai, China. Katika kipindi hicho wateja ambao watanunua Heineken watazawadiwa tiketi kwenda kwenye matukio ya kipekee ambapo wataweza kupiga picha za kombe hilo na hali kadhalika kupata fursa ya kuona uzoefu wa kandanda kupitia shughuli tofauti ambazo zitafanywa na Heineken. Sherehe inayohusisha watu maarufu (VIP) na wateja wa Heineken jijini Dar es Salaam itafanyika Machi 26 na 27, 2012.
Meneja Uhamasishaji wa Heineken, Hans Erik Tuijt, alisema, “Kila msimu wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Heineken inajitahidi kuwa na mazungumzo na mashabiki. Uzinduzi wa ziara hii ya Kombe la Mabingwa wa Ulaya kwa mwaka huu unawaleta karibu mashabiki wa mpira wa miguu duniani kwa tukio ambalo litawawezesha kujumuika na Heineken kwenye mashindano. Wakati tunakaribia kwenye fainali, tutaendelea kushikamana na mashabiki kwa kuonyesha uzoefu huu wa kihistoria.”
Akizungumzia kuhusu Ziara ya Kombe hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Matukio wa UEFA, David Taylor, alisema, “Ligi ya Mabingwa UEFA ina urithi wa muda mrefu na ni nguzo ya soka la vilabu vya Ulaya. Ziara ya Kombe hili kimsingi inaelezea ukweli wa jinsi ilivyokubalika duniani na mwitiko uliopo kwa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.”

No comments:
Post a Comment