Tangazo

March 27, 2012

Matukio Zaidi katika TBL Media Bonanza 2012

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mzee Samwel Sitta akiwapongeza wahariri waliofanya vizuri katika shindano la mbio za wahariri wakati wa Bonanza la Vyombo vya Habari lililoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na TBL, katika Klabu ya Msasani Beach jijini Dar es Salaam Machi 24.12. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto (kushoto kwa Waziri) ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo. Picha zote/John Badi

Wanahabari wa Business Times Limited wakisherehekea na kikombe baada ya kuibuka washindi wa jumla katika bonanza hilo.

PICHA YA KUMBUKUMBU: Mzee Sitta akiwa katika picha ya pamoja na Wanahabari (kutoka kushoto); Emmanuel Herman (Mwananchi), John Badi (ThisDay/Kulikoni & Daily Mitikasi Blog) na Mheshimiwa Lembeli (MB) Kahama.



Wanamuziki wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' wakilishambulia jukwaa.

Mnenguaji wa FM Academia akicheza sambamba na Mwanahabari Machachari, Iche Mang'enya.

No comments: