Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Machi 22.2012, kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 1 Aprili 2012, ambapo watatumia daftari lililotumika katika Uchaguzi wa Mwaka 2010 ambalo limefanyiwa marekebisho na kutumika katika Uchaguzi mdogo utakaowashirikisha jumla ya wapiga kura 127,455. Awali daftari la wapiga kura liliotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 lilikuwa na wapigakura 127,429 na baada ya marekebisho litakuwa na nyongeza ya wapiga kura 26 . Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Jullius Mallaba. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO) |
No comments:
Post a Comment