Tangazo

March 22, 2012

Polisi Konstebo Peter wa Trafiki Makao Makuu aibuka na Kitita cha Milioni 10/- za Vodacom M-Pesa

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Rene Meza akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Milioni 10/- kwa Mshindi wa Kwanza wa Mwezi wa Promosheni ya M-Pesa, Konstebo Peter James Kilalo (kulia) wa Makao Makuu ya Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City  jijini Dar es Salaam leo Machi 22.12. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya Milioni 10/- kwa Mshindi wa Kwanza wa Mwezi wa Promosheni ya M-Pesa, Konstebo Peter James Kilalo. Katikati ni  Mkurugenzi wa M-Pesa, Dylan Lennox.

Mshindi wa Kwanza wa Mwezi wa Promosheni ya M-Pesa, Konstebo Peter James Kilalo (kulia), akizungumza jambo huku akisikilizwa kwa makini na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Rene Meza na Maofisa wengine waandamizi wa Vodacom Tanzania.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Dylan Lennox akibadilishana na Mshindi Konstebo Peter James Kilalo.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Dylan Lennox (kulia), akijibu sehemu ya maswali ya waandishi wa habari.

Sehemu ya wafanyakazi wa Vodacom na waandishi waliohudhuria hafla hiyo.

No comments: