*****************
. Kituo hicho kitafaidisha zaidi ya watu 9,000 wa maeneo ya Bogoa, Shidi na Michenzani
. Airtel yakabidhidhi Mabati 264, Saruji 143, Nondo 62 na Mbao za kupau kituo cha Afya Michenzani
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbali mbali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kisiwani pemba maeneo ya michenzani kitakachosaidia kutoa huduma maeneo ya STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.
Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa Airtel Zanzibar Bw Hagai Samson alisema “msaada huu wa Airtel kwa wakazi wa huku pemba hautaishia hapa , leo tumejitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha afya tukiwa na imani vikitumika kwa usahihi vitasaidia kuboresha huduma za afya katika maene ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu, Kandandarani na Shidi.
Airtel Tanzania tunawashukuru sana wateja wetu mliopo pemba kwa kuwa ndio hasa wanaotuunganisha na jamii hii siku ya leo. Tunachojitolea hapa ni sehemu ya faida tunayoipata kila mnapozitumia huduma zetu zikiwepo kupiga na kupokea simu, Airtel money pamoja na huduma yetu ya Internet ya 3.75G.
Kwa upande wake Sheha wa Michenzani akipokea msaada huo wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho cha Afya aliishukuru Airtel na kuwaomba wadau wengine wanaofanya biashara kisiwani huko kuiga mfano huo wa Airtel.
“ naishukuru sana Airtel kwa msaada wao huu, utatusaidia sana kukamilisha ujenzi wa kituo hiki cha Afya hapa michenzani, tunaamini hii ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Ally M. Shein ambae wiki moja iliopita aliweka jiwe la msingi katika kituo hichi na kuhimiza ujenzi wa kituo hiki uende kwa kasi ili kusaidia kupunguza adha ya mrundikano wa wagonywa katika kituo kimoja kile cha Bogoa.
Nae Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani Omari Shehe Omari akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya una lengo la kupunguza matatizo ya afya yanayoikabili jamii inayoishi maeneo hayo hasa kwa kuzingatia wakina mama na watoto.
“Ninaipongeza Airtel sana kwa kujitolea na kutusaidia kufikia malengo yetu ya Milenia, sisi tuna dhamira ya kuboresha Afya na elimu kwa pamoja, kila Skuli iwe na kituo cha Afya au kila Shehia (Serikali ya Mtaa) iwe na kituo chake cha Afya.
Hivyo kwa msaaada huu utasaidia sana serikali yetu kutifika malengo yake kwamba pia michenzani watapata kituo chao hapa karibu.” Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ina mkakati wa kutoa misaada ya kijamii kwa kugusa sekta za mazingira, Elimu na Afya kwa lengo la kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla kupambana na changamoto mbalimbali .
Mwaka huu wa 2012 pia Airtel imejipanga kuhakikisha jamii iliyopo pembezoni mwa nchi mbali na kupata huduma bora ya mawasiliano ikiwemo ile ya Airtel money pia itashiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ili kujenga vyema ushirikiano na jamii kama ilivyoshiriki kuboresha miundombinu ya Afya Visiwani Zanzibar.

No comments:
Post a Comment