Tangazo

April 24, 2012

Rais wa Zanzibar apiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiwa katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kusiriki katika zoezi ya upigaji wa picha za vitambulisho vya Taifa,hapo jana sambamba  na utiaji saini fomu maalum na kuweka  alama za vidole,ikiwa ni utaratibu  wa ukamilishaji wa zoezi hilo (aliyesimama) Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Zanzibar Bw,Vuai Mussa Suleiman. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiweka  alama za vidole baada ya kupiga picha za vitambulisho vya Taifa,sambamba utiaji saini fomu za ukamilishaji wa zoezi hilo, zoezi hilo lilifanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kushoto) Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Zanzibar Bw,Vuai Mussa Suleiman (kulia), Mathayo Msungu,NIDA.  Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu Zanzibar

No comments: