XXXXXXXXXXXX
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuwatetea na kuwa upande wa wakulima kwa sababu ni jitihada zao ambazo zitaleta usalama wa chakula kwa maana ya chakula cha kutosha katika Afrika na kuzitoa nchi za Bara hili katika umasikini mkubwa.
Huo ndiyo ujumbe mkubwa wa Rais Kikwete wakati akiwa mjini Addis Ababa kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), Kanda ya Afrika, ambao kwa mwaka huu umefanyika kwa mara ya kwanza nchini Ethiopia.
Akizungumza kwenye kikao cha jana, Alhamisi, Mei 10, 2012, cha mkutano huo kilichozungumzia namna ya kuleta mageuzi katika Afrika – Grow Africa: Transforming African Agriculture, kilichofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton mjini Addis Ababa, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki wa mkutano huo:
“Wanunuzi na wafanyabiashara wa mazao siyo watu wenye huruma kabisa na mkulima. Bara letu litaendelea kuwa masikini na wakulima wetu wataendelea kuwa masikini kama hazitachukuliwa hatua za kumlinda mkulima dhidi ya mbinu za kuwapunja bei zinazobuniwa kila kukicha na wanunuzi wa mazao ambao ni watu katili na wasiojali ustawi wa mkulima.”
Rais Kikwete pia alitumia mchango wake kwenye mkutano huo kuelezea hatua ambazo ni muhimu katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika na mchango wa wahusika katika mchakato wa kuleta mageuzi hao zikiwamo Serikali, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa.
Mapema akizungumza na mwakilishi wa taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation, Bwana Lourie Lee, Rais Kikwete alitoa ujumbe kama huo kuhusu mageuzi ya kilimo katika Afrika akisisitiza kuwa Serikali yake wakati wote itakuwa upande wa wakulima na kuwatetea.
Rais Kikwete pia alimwambia Bwana Lee kuwa anafurahi kwamba Jumuia ya Kimataifa na hasa wafadhili wakubwa duniani wameanza tena kuonyesha nia na dhamira thabiti kuunga mkono maendeleo ya kilimo.
“Hali inatia moyo sana. Kama unavyojua kuna wakati wafadhili walikuwa wanatoa kiasi cha dola bilioni 18 kuendeleza kilimo katika Afrika. Lakini idadi hiyo ilishuka na kufikia dola bilioni tatu. Nafurahi kuona kuwa kiasi hicho kimeongezeka na kufikia dola bilioni sita kwa sasa kwa sababu bila uwekezaji wa maana, kilimo cha Afrika kitaendelea kuwa duni na cha kujikimu.”
Aliongeza Rais Kikwete: “Ukweli ni kwamba ukipuuza kilimo, dunia haitaweza kujihakikisha usalama wa chakula na pia hatutaweza kuwatoa mamilioni ya watu wa Afrika kutoka kwenye umasikini kwa sababu kilimo ni mwajiri mkuu katika Bara hili.”
Mbali na kukutana na Bwana Lee, Rais Kikwete pia alikutana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Kofi Annan ambaye taasisi yake inajihusisha na jitihada za kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
11 Mei, 2012
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mageuzi yoyote ya kilimo katika Afrika ni lazima yalenge katika kumlinda mkulima dhidi ya walanguzi, wachuuzi na wafanyabiashara wa mazao ambao amewaelezea kama watu katili na wasiojali ustawi wa mkulima.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuwatetea na kuwa upande wa wakulima kwa sababu ni jitihada zao ambazo zitaleta usalama wa chakula kwa maana ya chakula cha kutosha katika Afrika na kuzitoa nchi za Bara hili katika umasikini mkubwa.
Huo ndiyo ujumbe mkubwa wa Rais Kikwete wakati akiwa mjini Addis Ababa kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), Kanda ya Afrika, ambao kwa mwaka huu umefanyika kwa mara ya kwanza nchini Ethiopia.
Akizungumza kwenye kikao cha jana, Alhamisi, Mei 10, 2012, cha mkutano huo kilichozungumzia namna ya kuleta mageuzi katika Afrika – Grow Africa: Transforming African Agriculture, kilichofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton mjini Addis Ababa, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki wa mkutano huo:
“Wanunuzi na wafanyabiashara wa mazao siyo watu wenye huruma kabisa na mkulima. Bara letu litaendelea kuwa masikini na wakulima wetu wataendelea kuwa masikini kama hazitachukuliwa hatua za kumlinda mkulima dhidi ya mbinu za kuwapunja bei zinazobuniwa kila kukicha na wanunuzi wa mazao ambao ni watu katili na wasiojali ustawi wa mkulima.”
Rais Kikwete pia alitumia mchango wake kwenye mkutano huo kuelezea hatua ambazo ni muhimu katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika na mchango wa wahusika katika mchakato wa kuleta mageuzi hao zikiwamo Serikali, sekta binafsi na mashirika ya kimataifa.
Mapema akizungumza na mwakilishi wa taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation, Bwana Lourie Lee, Rais Kikwete alitoa ujumbe kama huo kuhusu mageuzi ya kilimo katika Afrika akisisitiza kuwa Serikali yake wakati wote itakuwa upande wa wakulima na kuwatetea.
Rais Kikwete pia alimwambia Bwana Lee kuwa anafurahi kwamba Jumuia ya Kimataifa na hasa wafadhili wakubwa duniani wameanza tena kuonyesha nia na dhamira thabiti kuunga mkono maendeleo ya kilimo.
“Hali inatia moyo sana. Kama unavyojua kuna wakati wafadhili walikuwa wanatoa kiasi cha dola bilioni 18 kuendeleza kilimo katika Afrika. Lakini idadi hiyo ilishuka na kufikia dola bilioni tatu. Nafurahi kuona kuwa kiasi hicho kimeongezeka na kufikia dola bilioni sita kwa sasa kwa sababu bila uwekezaji wa maana, kilimo cha Afrika kitaendelea kuwa duni na cha kujikimu.”
Aliongeza Rais Kikwete: “Ukweli ni kwamba ukipuuza kilimo, dunia haitaweza kujihakikisha usalama wa chakula na pia hatutaweza kuwatoa mamilioni ya watu wa Afrika kutoka kwenye umasikini kwa sababu kilimo ni mwajiri mkuu katika Bara hili.”
Mbali na kukutana na Bwana Lee, Rais Kikwete pia alikutana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Kofi Annan ambaye taasisi yake inajihusisha na jitihada za kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Mheshimiwa Paschal Lamy, Mheshimiwa Beverly Oda ambaye ni Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Canada na Bibi Elizabeth Buze, Rais wa Kundi la Makampuni ya Visa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
11 Mei, 2012
No comments:
Post a Comment