Tangazo

June 28, 2012

Msanii Nyota wa Bongo Movie, Ray Kigosi azindua Filamu yake Mpya ya 'Sobbing Sound' kwa Kutoa Misaada kwa Watoto Yatima


Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni, Bi. Zainabu Bakari ambapo vyakula vya aina mbalimbali vimetolewa vyenye thamani ya Milioni 1.5/-.  Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage. Picha na Mpiga picha Wetu
 ******************
 MSANII wa filamu nchini  Visent Kigos 'Ray'  amezindua filamu yake  mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.

Filamu hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5/-  kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo,  Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba  watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutahabika kitendo ambacho si kizuri.

" Ujio wa filamu hii ni kama azma yangu niliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zangu zote zinafanya vizuri na ntakuwa kila filamu ntakayotoa nitahakikisha japo kidogo kwa namna yoyote nawakumbuka watoto yatima kwani nawajapenda",  alisema.

Aidha alibainishwa kuwa kampuni ya  Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kuwashawishi wawe wanawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage amesema swala la watoto yatima ni letu sote na wala halichagui kwa kuwa tuna wajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukrani zetu.

Msanii wa Filamu Vicent Kigosi 'Ray' na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja watoto.

No comments: