Tangazo

July 4, 2012

HUDUMA ZAENDELEA KUIMARIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI


Leo huduma za tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimeendelea kuimarika katika maeneo mengi. Taarifa kutoka Kurugenzi ya Tiba (idara ya tiba, idara ya magonjwa ya dharura, idara ya wagonjwa wa nje, idara ya magonjwa ya afya ya akili, na idara ya watoto) na Kurugenzi ya Upasuaji (idara ya upasuaji, idara ya magonjwa ya wanawake, idara ya meno, idara ya magojwa ya masikio, pua na koo, idara ya macho, na idara ya nusu kaputi) imeonyesha kuimarika kwa huduma kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na hali ilivyokuwa siku chache zilizopita. Ifuatayo ni thathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa 2:00 hadi saa 11 jioni leo tarehe 4 Julaiy, 2012.

Kurugenzi ya Tiba
Idara ya Tiba: (Internal Medicine)
Madaktari walioko katika mafunzo kwa vitendo (Interns) 11wamefika kazini na kufanya kazi. Registrar’s wote wamefanya kazi, Madaktari Bingwa wote wamefanya kazi. Service ward rounds zimefanyika pamoja na kliniki ya HIV imefanyika.

Idara ya Magonjwa ya Dharura: (Emergency Medicine)
Madaktari waliokuwepo  ni Daktari Bingwa mmoja, Registrars wawili na pamoja na Interns wawili.

Idara ya Wagonjwa ya Nje (Cold OPD)
Registrars wote walikuja kazini na wawili wana ruhusa maalum. Wagonjwa wote waliofika walionwa.

Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili (Psychiatry and Mental Health)
Madaktari Bingwa wote walikuwepo kazini isipokuwa mmoja ambaye yuko masomoni. Kliniki zote zimefanyika, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa

Idara ya Watoto: (Pediatrics and Child Health) 
Madaktari Bingwa wote wamekuja kazni na kufanya kazi.  Interns watatu nao walikuja na kufanya kazi.

Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) 
Huduma kwa wagonjwa wote waliolazwa chumba cha wagojwa mahututi wameonwa  na wanaendelea kuhudumiwa chini ya uangalizi wa karibu..

Kurugenzi ya Upasuaji
Upasuaji leo umefanyika na kuna ongezeko kubwa la madaktari lililojitokeza leo kwa ajili ya kufanya upasuaji katika vyumba vya upasuaji. Orodha ya wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji kesho Alhamisi Julai 4, 2012 imeandaliwa na wagonjwa wote wamefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya upasuaji ikiwemo kushauriwa na kukubali kufanyiwa upasuaji, kupimwa viwango au wingi wa damu kama inatosha mgonjwa kufanyiwa upasuaji pamoja na taratibu nyingine za tiba. Hata hivyo, wagonjwa bado ni wachache wanaokuja kliniki na waliolazwa wodini.

Idara ya Upasuaji: (General Surgery)
Idara ya Upasuaji wagonjwa walionwa na Madaktari bingwa tu, hapakuwa na Interns wala Residents. Kliniki zote zilizopangwa kufanyika leo zimefanyika hususani kliniki ya masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya wanawake, macho (ophthalmology), matumbo (gastroentology), njia ya haja ndogo kwa wanaume (urology), ngozi (skin), ART, magonjwa ya moyo (cardiovascular), meno, plastic surgery pamoja na pediatric surgery. Aidha kliniki zote kwa ajili ya wafanyakazi na wagonjwa wa kulipia (private) zote zimefanyika

Idara ya Magonjwa ya Wanawake: (Obstetrics and Gynaecology)
Wagonjwa wote waliolazwa wameonwa na Madaktari Bingwa kwa kushirikiana na Interns wachache waliokuwepo.

 Idara ya Meno: (Dental Surgery)
Madaktari waliokuwa zamu walipita round na waliona wagonjwa wote waliolazwa.

Idara ya Masikio, Pua na Koo: (Otorhinolaryngology)
Makaktari Bingwa walipita wodini kuona wagonjwa waliolazwa na kufanya upasuaji kwa wagonjwa wawili.

Idara ya Nusu Kaputi: (Anaesthesia)
Madaktari Bingwa na wasaidizi wao walikuwepo na kuendelea na kazi kama kawaida.

 Idara ya Macho: (Ophthalmology)
Madaktari Bingwa waliona wagonjwa wote waliolazwa wodini, waliendelea, kliniki na kufanya  upasuaji.

 Vyumba vya upasuaji: (Theatre)
Urology:  Walikuwa na  orodha ya upasuaji na walifanya upasuaji wa mtu mmoja.
Pediatric Surgery:          Hawakuwa na orodha ya upasuaji kwa siku ya leo
Plastic Surgery:             Hawakuwa na orodha ya upasuaji.
Otorhinolaryngology (ENT): Walikuwa na orodha, walifanya upasuaji kwa  wagonjwa wawili.
    Macho:                         Wamefanya zote zilizotakiwa

Kurugenzi ya Tiba Shirikishi (Clinical Support Services) 
Madaktari wa Radiolojia wote nane walikuwepo kazini na wamefnya kazi. Hata hivyo eneo hili halikuwa katika mgomo. Upande wa Maabara: huduma zote ziliendelea kutolewa. Pia eneo hili halikuwa katika mgomo.

Idara ya Pharmacy yenye iliendelea kufanya kazi na pia haikuwa katika mgomo. Idara hii pia ina   Interns 30 na kati yao watatu wako likizo mmoja yuko likizo ya uzazi waliobaki 27 wote walikuwa kazini na kuchapa kazi.

Idara hii ina Wafamasia 12 ambapo 10 kati yao walikuwepo, na wawili wana likizo maalumu. Pharmacy zote zimefunguliwa na kufanya kazi. Eneo hili pia halikuwa kwenye mgomo.

Kurugenzi ya Uuguzi na Ubora (Nursing Services and Quality)
Wauguzi wote wanaotakiwa kuwepo kazini wapo na wanaendelea na kazi. ha

Tathimini ya jumla:
Huduma zimeendelea kuimarika. Wagonjwa ni wachache. Madaktari wengi wamerudi kazini na wanachapa kazi.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 4, 2012

No comments: