Tangazo

July 20, 2012

Ngoma Africa Band yatoa Salamu za Rambi Rambi kutokana msiba wa ajali ya Meli ya MV Skagit

Bendi ya Muziki "Ngoma Africa band" yenye makao Ujerumani, Inatoa pole na rambi rambi kwa ndugu na jamaa wote waliopatwa msiba kutokana na jali ya meli ya MV Skagit,iliyotokea jana 18-7-2012 jirani na Chumbi, Zanzibar.

Ngoma Africa Band inaungana na watanzania wote walio nyumbani na  nje ,katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa kitaifa,msiba huu ni wetu sote. Katika maombelezo bendi inasimamisha shughuli zake kwa muda wa wiki moja.

Mungu Ibaraki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika

No comments: