Tangazo

August 24, 2012

KARAKANA YA WONDER YANUFAIKA NA VYUMA CHAKAVU KUTOKA TBL


Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akiwasaidia wafanyakazi wa Karakana ya Wonder,Nico Ngalawa (kulia) na Hafidh Selemani wakipakia kwenye gari vyuma chakavu walivyopewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), vilivyokusanywa juzi katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Ilala Mchikichini, Dar es Salaam.

Baadhi ya sanamu zilizotengenezwa kwa kutumia vyuma chakavu zikiwa zimepambwa katika moja ya bustani katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mfanyakazi wa Wonder Workshop akijiandaa kuchonga chupa ili kupata bilauri hivi karibuni katika karakana hiyo.

Wafanyakazi wa Karakana ya Wonder wakinyanyua moja ya nembo (logo) iliyotengezwa kwa vyuma chakavu.

Fundi Mchundo (Welder), Seif Chambela akiwa na sanamu ya tembo iliyotengenzwa kwa kutumia vyuma chakavu katika Karakana ya Wonder (Wonder Workshop)Wafanyakazi wa Karakana ya Wonder (WonderWorkshop), Msasani, Dar es Salaam.

Meneja Mradi wa Wonder Workshop, Lisette Westerhuis akimuonyesha Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi, sanamu ya ndege aliyetengenezwa kwa kutumia vyuma chakavu katika karakana hiyo iliyopo Msasani jijini Dar es Salaam hivi karibuni. TBL itakuwa inaipatia kila mara Karakana hiyo vyuma chakavu na makasha kwa ajili yakutengenezea vifaa mbalimbali zikiwemo sanamu za wanyama.

No comments: