Tangazo

August 6, 2012

TBL YASAIDIA VISIMA 15 VYA MAJI KATIKA VIJIJI VYA WILAYA YA LUDEWA

Katibu Tarafa wa Ngelenge, Januari Mwambeleko akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa visima 15 vilivyojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika baadhi ya vijiji wilayani Ludewa, Mkoa mpya wa Njombe. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni wilayani humo. (NA MPIGAPICHA WETU)

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya maofisa wa TBL pamoja na viongozi wa vijiji wilayani Ludewa walionufaika na mradi huo.

Mwambeleko akipampu maji kwenye moja ya visima hivyo.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Ngelenge, Kata ya Manda,wakati wa uzinduzi wa visima 15 vilifadhiwa na TBL, wilayani Ludewa, Mkoa waNjombe hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo akinywa maji kuashiria kuwa ni safi na salama kwa matumizi ya binadamu katika hafla ya kukabidhi mradi wa visima 15 wilayani Ludewa, Mkoa waNjombe hivi karibuni. Mradi huo umefadhiliwa na TBL.

No comments: