Tangazo

October 21, 2012

MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI KIGOMA

Timu ya Katonga A ambao ni mabingwa wa mkoa wa Kigoma wakimaliza mashindano ya kupiga makasia ya Bia ya Balimi kwenye Ziwa Tanganyika.

Mabingwa wa mashindano ya Balimi boat race mkoa wa Kigoma upande wa wanawake Timu ya Upendo. 

Meneja wa Bia ya Balimi, Edith Bebwa (kulia) akishuhudia namna wachezaji wa timu mbalimbali walivyokuwa wakitoana jasho kwenye fainali ya Mashindano ya Kupiga makasia ya Bia ya Balimi kwenye ziwa Tanganyika.

Mabingwa wa mashindano ya Balimi boat race mkoa wa Kigoma upande wa wanaume Timu ya Katonga A wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya 900,000/- kama zawadi ya ushindi wa kwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhani Maneno (kushoto), akimkabidhi kitita cha 700,000/- Kapteni wa timu ya Wanawake ya Upendo, Bi. Mawazo Shaban Juhudi mara baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hiyo.

No comments: