Tangazo

November 14, 2012

MULTICHOICE ILIPOTANGAZA PUNGUZO LA MALIPO YA MWEZI KWA 10%


Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel, akitangaza Punguzo la Asilimia Kumi ya Malipo ya mwezi kwa wateja wa Televisheni kwa Vipindi vya DStv likaloanza hapo kesho, ambapo amesema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma za Matangazo ya Televisheni ya kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia amesema Offer hiyo ya Punguzo la bei ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kuelekea katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Barbara Kambogi na Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu.

Meneja Masoko wa Multichoice wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu akitoa ufafanuzi kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea matumizi ya mfumo wa Digitali DStv kwa kuwajali wateja wake imepunguza gharama za kuunganishwa ambapo sasa ni kwa shilingi za Kitanzania 169,000 unaweza kusheherekea msimu wa sikukuu na DStv.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akiwahakikishia wateja wa DStv kuwa sasa kampuni hiyo imezidi kuboresha huduma zenye viwango vya hali ya juu na kuwataka wazazi kutumia fursa hii ya punguzo la bei ya kuunganishwa ili watoto wao waweze kushuhudia vipindi mbali mbali vya kuelimisha na kuburudisha ikiwemo filamu kali, katuni maridadi, michezo mbalimbali katika kipindi hiki cha likizo kwa watoto wao na kuwa huu ndio sasa muda muafaka kwa kujipatia DStv.

Meneja Mauzo wa DStv Tanzania Bw. Salum Salum akifafanua kuwa Multichoice imepanua wigo wa kutoa huduma kwa wateja ambapo sasa wanamawakala 200 nchini na kuwataka wanapokwenda kulipia Ving'amuzi vyao ni lazima wahakikishe vimewashwa ili kurahisisha kufanyika kwa huduma hiyo pia amesema wateja wa DStv wanaweza kufanya malipo ya huduma hiyo kupitia simu za mkononi na ukizingatia kampuni hiyo imeongeza maeneo ya kutoa huduma ikiwemo Uchumi Super Market, Kariakoo na Mlimani City kwa wakazi wa Dar es Salaam.

No comments: