Tangazo

April 9, 2013

Kampeni ya kusafisha Jiji ya Green Waste Pro yakabiliwa na changamoto


Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie.
Baadhi ya Dust bin zinazomilikiwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd. zilizowekwa katika baadhi ya mitaa ya Manispaa ya Ilala ambazo pia mteja yoyote anapohitaji huuzwa.
Na.Mwandishi wetu.

Wananchi wa jiji la Dar es Salaam hususan wakazi wa manispaa ya Ilala wametakiwa kutambua kuwa suala la usafi na kutunza mazingira ni jukumu la watu wote na sio tu la kampuni zilizopewa kandarasi ya kukusanya taka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd iliyopewa dhamana ya kufanya usafi katika manispaa ya Ilala Vidah Fammie amesema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku wanakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo watu kutochangia katika ulipaji wa ada ya taka na pia kutolipa kwa muda muafaka.

Akiendelea kuzitaja changamoto hizo amesema pia wangependa wananchi watambua kuwa suala la dust bin, watu wamekuwa wakielewa vibaya kuwa wao ndio wanaopaswa kuzimbaza jambo ambalo sio kweli, kampuni ya usafi ya Green Waste Pro wanaziuza na hawamlazimishi mteja wao yeyote kununua, ila anaruhusiwa kununua pale anapopenda, na kuwa zile dust bin zinazowekwa mitaani wao wanapata usaidizi kutoka manispaa.

Pia ameshauri kwa wale ambao hawana dust bin watumie mifuko maalum ya kuweka taka na gari litakapopita litachukuwa kama ulivyo utaratibu wa suala la usafi.

Bi. Vidah Fammie ameongeza kuwa tatizo jingine wanalokabiliana nalo ni suala la upeo mdogo wa wananchi kuhusu suala la usafi.

Mwandishi wa habari hizi alipotaka ufafanuzi kuhusu suala hilo, amesema inaonekana wapo wananchi wanaoelewa suala zima la usafi lakini wanapuuzia na kuna wale wasio elewa kabisa hivyo mtu akiwa na taka anatupa tu kwa kuwa anajua kuna mkandarasi wa kufanya usafi kitu ambacho si sawa.

Kingine amesema ni miundo mbinu mibovu na hali ya hewa hivyo wakati mwingine kwa mfano gari maalum la kusafisha barabara linashindwa kufika hivyo inabidi kutumika nguvu za ziada kama vile vibajaji na vitu vingine.

No comments: