Ngassa atambulishwa Rasmi Yanga; Amwaga wino Miaka Miwili
Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako amemtambulisha rasmi Mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kuwa mchezaji mpya kujiunga na timu hiyo msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa.
Mrisho Ngassa akiibusu jezi ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi kurejea katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili asubuhi ya leo, makao ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog
No comments:
Post a Comment