Tangazo

May 20, 2013

Waziri Membe ateta na Mabalozi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akiongea na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam alipokutana nao kujadili maandalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) na mchango wao katika kuhamasisha ushiriki wa nchi wanazotoka katika mkutano huo utakaofanyika mwezi ujao. Kushoto kwake ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Juma - Alfani Mpango.

Meneja Mradi wa maandalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao kuhusu maendeleo na maandalizi ya mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika mwezi June jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais 10 kutoka nchi zilizoendelea.
 

Sehemu ya mabalozi wakifuatilia hatua mbalimbali za maandalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) na mchango wao katika kuhamasisha ushiriki wa nchi wanazotoka katika mkutano huo. Zaidi ya washiriki 500 wanatarajiwa kwenye mkutano huo utakaojadili kwa kina matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuleta Maendeleo kwa nchi zinazoendelea.


Meneja Mradi wa mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano kwa manufaa ya Wote (Smart Pertinership) Rosemary Jairo akitoa ufafanuzi kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao leo jijini Dar es salaam kuhusu maendeleo na maandalizi ya mkutano huo utakaohudhuriwa na wachumi, wanasayansi na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka ndani na nje ya nchi. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments: