Tangazo

September 29, 2013

KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMANI TANZANIA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waumini wa kanisa la TGMIT lililopo Mwanza, Katibu wa NEC aliwaeleza waumini waliohudhuria ibada hiyo maalumu kuwa amani tuliyokuwa nayo imeletwa na Mwenyezi Mungu hivyo tusiruhusu ipotee.
 Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la TGMIT Florence Ndaki akiongoza ibada maalumu ya kuiombea Tanzania amani, katika ibada hiyo viongozi mbali mbali walialikwa kutoka serikalini ,vyama vya siasa na asasi zisizo za kiserikali.
Waimbaji wa Kwaya maarufu nchini Martha Ramadhani na Mary Ruhasha wakiimba wimbo maalum wa kuitakia amani Tanzania kwenye ibada maalumu iliyofanyika leo tar.29 September 2013 kwenye knisa la TGMIT Mwanza.
Waumini wa Kanisa la TGMIT  Mwanza wakiwa kwenye maombi maalum ya kuiombea Tanzania amani, ambapo Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye alikuwa mgeni mwalikwa na viongozi wengine kutoka serikalini,asasi zisizo za kiserikali na vyama vingine vya siasa.

Serikali yabariki Tamasha la Utamaduni Handeni

Na Mwandishi Wetu, Handeni

SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dr Khalfany Haule (PICHANI), imebariki kufanyika kwa tamasha la utamaduni la Handeni Kwetu 2013, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani humo.

Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango wenye mashiko kwa sekta hiyo.

Akizungumza juzi mjini hapa, Dr Haule alisema ni kitendo kinachopaswa kuungwa mkono na serikali yote ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwa kupitia njia mbalimbali.

Alisema wao kama wilaya wamepokea kwa mikono miwili wazo zuri la kuandaliwa kwa tamasha hilo wilayani Handeni mkoani Tanga, hivyo watakuwa pamoja na waandaaji.

“Tunashukuru kwa dhati kuona mwaka huu mwishoni kunafanyika tamasha hili lenye mguso wa aina yake, maana watu watakutana kuangalia mambo ya utamaduni wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.

“Tupo tayari kushirikiana kwa karibu na waandaaji wa tamasha hili ili lifanyike kwa mafanikio na kuleta ari mpya katika sekta ya maendeleo ya Taifa, hususan wilayani Handeni,” alisema Haule.


Tamasha la Utamaduni wa Handeni linafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuandaliwa na Raha Company And Entertainment likiwa na malengo ya kukuza na kutangaza sekta ya utamaduni na utalii hapa nchini na kusubiriwa kwa hamu wilayani humo.

IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA NANE TANZANIA

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
 Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecelaamesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

 Daktari. Mwelecele Malecela ameimabia Father Kidevu Blog, katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam kuwa mkutano huo unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari. Hussein Mwinyi.
Makamu huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.

"Mkutano pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).

Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii" 

Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.

WASHIRIKI ZAIDI YA 100 NDANI NA NJE YA NCHI KUKUTANA KATIKA TAMASHA LA SANAA LA JAMBO FESTIVAL

ZAIDI ya  washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba 23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini hapa.

 Mwenyekiti wa tamasha hilo, la Jambo Festival 2013 ,Augustine Namfua alisema kuwa , tamasha hilo ni la pili kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni kuwawezesha  washiriki mbalimbali kuweza kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa, tamasha hilo ambalo ni la kimataifa pia litawashirikisha washiriki kutoka nchi za Ufaransa,na Angentina ambao wataweza kuonyesha matamasha mbalimbali ya kitamaduni sambamba na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni  .

Alisema kuwa, tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili ikiwemo maonyesho  ya mavazi ya kiasili,pamoja na tamasha la kiasili kutoka vikundi jijini Tanga, Arusha,  na Dar es Saalamu .

 Namfua aliongeza kuwa, pia kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa    pamoja na onyesho la  mavazi , na ubunifu wa mavazi ambapo  katika tamasha hilo kwa siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali ambayo yatakuwa yakionyeshwa .

 Aliongeza kuwa, tamasha hilo limekamilika kwa asilimia 50 huku watu mbalimbali wakiwemo binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo .

 ‘tamasha la mwaka jana lilifana sana kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku watu mbalimbali wakipata fursa ya kuonyesha sanaa zao na tamaduni mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi ndio maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi hivyo tunatarajia  watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha hilo’alisema Namfua.

 Aidha aliwataka watu mbalimbali kufika katika tamasha hilo na kuonyesha  bidhaa zao za kitamaduni zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza tamaduni zao za kiafrika , huku akiwataka wadau mbalimbali kuonyesha  moyo katika kusaidia matamasha hayo  ili yaendelee kufanyika mara kwa mara.

September 26, 2013

ZIARA YA KINANA MKOANI MARA YAMALIZIKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya sanamu ya mfano wake kutoka kwa Ndugu Elia Bugurilo Kamoga.

Josephat Amon Muruga akiwa na wenzake sita baada ya kujiunga na CCM wakitokea Chadema.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa anavuka na kivuko cha MV Musoma kutoka Kinesi kuelekea Musoma mjini,Kivuko hicho ambacho kimekuwa  mkombozi  wa usafiri kinauwezo wa kubeba abiria 330.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu vazi la kujiokoa wakati wa hatari wakati wa kuvuka  na kivuko cha MV Musoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Balozi wa shina namba 6 Tabitha Edgar wa kata ya Kitagi.
Balozi wa nyumba kumi Tabitha Edgar wa shina namba 6 kata ya Kitagi akitoa shurani zake za kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abbulrahman Kinana.
Katibu Mkuu akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria uliopo eneo la Bukanga(Makoko) mradi huo utakamilika katikati ya mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji huku akipatiwa maelezo na mhandisi Jairos Chilema ,mradi huo utakuwa na bomba kubwa la kilomita tisini na ukikamilika utaondoa kabisa tatizo la maji Musoma Mjini.

TBL YAWEZESHA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KATIKA MIKOA YA MOROGORO NA PWANI

 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi (wa pili kulia) na dereva wa kampuni ya Tasia Hogistic ya jijini Dar es Salaam, Verry Philiph (39) wakikabidhiwa cheti baada ya kupimwa shinikizo la damu na wateknolojia wa maabara wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Theodol Babwanga kushoto na Daniel Mwita wakati mkuu huyo alipozindua mpango wa upimaji wa afya kwa madereva wa malori makubwa katika mizani ya Mikese kufuatia kampuni ya TBL kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wa malori ikiwa kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikibeba ujumbe wa "usalama unaanza kwangu kisha kwako na sisi sote" mkoani Morogoro.Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL. Steve Kilindo.

 Mkuu wa Usalama Barabarani Chalinze, Innocent Sule akiwa anazungumzana baadhi ya madereva wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya mikoa ya Dar es Salaam na Arusha zoezi lililofanyika katika mizani ya
Kiangaiko iliyoko Msata Bagamoyo. Kampuni ya Bia Tanzania TBL, sh. mil. 13 kwa uongozi wa Hospitali Teule ya Tumbi kwa lengo la kufanikisha kupima madereva wanaotarajiwa kufikia 800 ikiwa na lengo la kupunguza kama si kumaliza ajali.

Mmoja wa madereva akichukuliwa vipimo na daktari
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi kushoto na dereva wa kampuni ya Tasia Hogistic ya jijini Dar es Salaam, Verry Philiph (39) kulia wakipimwa shinikizo la damu na wateknolojia wa maabara wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Theodol Babwanga kushoto na Daniel Mwita wakati mkuu huyo alipozindua mpango wa upimaji wa afya kwa madereva wa malori makubwa katika mizani ya Mikese kufuatia kampuni ya TBL kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wa malori ikiwa kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikibeba ujumbe wa "usalama unaanza kwangu kisha kwako na sisi sote" mkoani Morogoro. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL. Steve Kilindo.

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ahmed Kipozi (kulia) akizungumza na mmoja wa Daktari wakati alipokwenda kushuhudia zoezi la upimaji afya kwa madereva, makondakta na watu mbalimbali kwenye siku ya kwanza ya wiki ya nenda kwa usalama ambayo imefanyika katika mizani ya Kiangaiko iliyoko maeneo ya Msata Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.Katikati ni Meneja Uhusiano wa TBL,Doris Malulu.

September 25, 2013

Kibonzo cha Leo... Tanzania Je??


ENZI HIZO... HIVI SASA INAWEZEKANA?


The legend is back first anniversary

Sasa zimebaki siku 4 tu kabla ya kufika siku tunayoisubiri kwa hamu, The Legend is Back first anniversary. Project ilianza kwa support yenu na ni mwaka sasa tunatimiza kwa sapport yenu. 

Tulianza pamoja karibu tujumuike tutimize mwaka tukiwa pamoja. Siku hii muhimu itaambatana na shindano kali la disco dancing toka kwa mabingwa wa zamani kuiwakilisha Morogoro Maneno Ngedere na toka DSM Athuman Diga Diga. 

Vile vile wakali wa chacha Africa Mashariki Moddy Jazz B na Sunday Boy watachuana vikali. Utakuwa vilevile na special moment of silence kuwakumbuka malegendari wa disco waliotutangulia mbele ya haki ni j'mosi hii 28/9/2013 ndani ya isumba lounge. Wote mnakaribishwa.

KITABU CHA MWONGOZO WA UTAWALA BORA CHAZINDULIWA

Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki akizindua Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki akionesha kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” alichokizindua leo makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya  Katiba na Sheria Angellah Kairuki  akiongea na washiriki waliohudhuria uzinduzi wa kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” leo katika ofisi za  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) zilizopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyeki wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Amiri Manento (Jaji Kiongozi Msaafu).
Mwenyeki wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Amiri Manento (Jaji Kiongozi Msaafu) akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es Salaam. (Katikati) ni Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki, Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyeki wa THBUB Mahfoudha Alley Hamid.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mary Massay akiwasisitiza washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika katika ofisi za THBUB zilizopo mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es Salaam. Wakwanza ni ni Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki (katikati) ni Mwenyeki wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Amiri Manento (Jaji Kiongozi Msaafu).
Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)

Serikali kuanzisha benki ya vijana

NA MAGRETH   KINABO- MAELEZO
 
SERIKALI ina mpango wa kuanzisha benki ya vijana amabyo itakuwa ikiwapatia mikopo nafuu  ili kuwawezesha  kujiajiri  wenyewe  ikiwa ni hatua ya kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.

Kauli  hiyo imetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (pichani), wakati wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu na jinsi kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ,jijini  Dares Salaam.

Makamu  huyo wa Rais  alisema hayo kufutia chapisho hilo kuonesha kwamba  kundi la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi miaka 35 kuwa ni watu milioni 15.6 sawa na asiliamia 34.7 ya watu wote nchini.

“ Idadi hii ya vijana ikitumiwa vizuri itaongeza uzalishaji na hatimaye kukuza uchumi  wa nchi na kupunguza umasikini ,” alisema Balozi Seif.

 Aliongeza kuwa Serikali na watu wengine wataendelea kuifanya Sera ya Maendeleo ya   Vijana ya mwaka 2007, ikiwemo kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali ni mojawapo ya mikkati ya kuendeleza vijana.

“ Kwa kuzingatia rasilimali zilizopo Serikali ina dhamira ya Kuimarisha viwanda na Kilimo Kwanza kama njia nyingine za kuwazesha vijana kupata ajira na kuongeza kipato. Vijana wa tabia ya kungojea ajira kazi za maofisi ambazo haziko nyingi, bali wajiunge na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujaipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao,” alisisitiza.

 Aidha aliongeza  kwamba kupitia  chapisho hilo, limeonesha kuwa kundi jingine la wazee wenye umri wa  miaka 60 au zaidi amabo ni milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya watu wwote nchini. Hivyo kulingana na Sera  ya Wazee kundi  hilo  linahitaji huduma maalum kama vile, matibabu, malazi na huduma nyingine muhimu.

“Serikali  na wadau wengine wataendelea kuwapatia wazee hawa huduma muhimu kulingana na hali ya uchumi wan chi,” alisema.

 Balozi Seif alizita  Wizara ,Idara na Taasisi zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha sera zilizopo  na kutumia takwimu hizi katika kupanga mipango ya maendeleo.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Dk. Albina Chuwa alisema  chapisho hilo linaonesha kuwa umri  unaoanzia miaka 0 hadi 4  kuashiria kuwa kiwango cha  uzazi bado ni kikubwa.

 Alifafanua kuwa kwa kumujibu wa Utafiti wa  Mama na Mtoto wa mwaka 2010 kiwango cha uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama mwenye umri wa miaka 15hadi 49, hivyo  uzazi wa mpango utaendelea kusisitizwa.

Naye Mwakilishi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia (UNFPA)Mariam Khan alisema chapisho hilo  litasaidia kujua iddai ya watu wanaojiandikisha shule, wastaafu, kupanga  uzazi wa mpango na mipango mingineyo.

CCM YATIKISA SHIRATU

  • KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE
  • MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU
  • VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI
  • WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO

 Mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu waliofurika kwenye uwanja wa Shiratu Obwere,Mbunge huyo alieleza jinsi gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na mshikamano walio nao.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu wilaya ya Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata taratibu zote za kisheria.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa CCM inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya ,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na itakayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala zima la mradi wa umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
 Sehemu ya Umati wa watu walifurika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Shiratu Obwere tarehe 24 Septemba 2013.


BLOG MPYA MAALUM KWA VIDEO ZA BONGO TU - ONLY FOR BONGO VIDEO'S

KUTOKA KAPITALI ONLINE MARKETING & ADVERTISING COMPANY INAWALETEA BLOG HII MAALUM KWA AJILI YA MUSIC WA BONGO TU, LIVE SHOW ZA WASANII WA BONGO NA INTERVIEW ZAO.

UKITEMBELEA BLOG HII UTAWEZA KUPATA VIDEO ZOTE KALI ZA BONGO NA MATUKIO YANAYOHUSU WASANII KWA VIDEO.

KWA WASANII WANAOHITAJI VIDEO ZAO ZIWEKWE KWENYE HII BLOG WANAWEZA 
WASILIANA NASI KWA

EMAIL: videozabongo@gmail.com
BLOG: www.videokalibongo.blogspot.com
PIA TUNAFANYA VIDEO PROMOTION

ZIARA YA PINZA LOLIONDO - NGORONGOR0

Mmoja wa wananchi  wa kijiji cha Mdito wilayani Ngorongoro akiwa na bango la kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kijijini hapo akiwa  katika  ziara ya wilaya  hiyo Septemba 24, 2013. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akivalishwa zawadi ya shanga na Bibi  Martha Seleli  wa kijiji cha Mdito wilayani Ngorongoro wakati  Waziri  Mkuu , Mizengo  Pinda alipopita kijijini hapo akiwa katika ziara ya wilaya hiyo.

Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akisalimiana na Babu wa Loliondo.

Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akiwa na wacheza ngoma wa kabila la Wasonje  kabla ya kuhutubia mkutano wa  hadhara katika kijiji cha Digodigo wilayani Ngorongoro   Septemba 24, 2013.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  (kulia)  akicheza  ngoma na wasichana wa  kabila la Wasonje  wakati Waziri Mkuu, Mizengo  pinda alipohutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Digodigo  wialyani Ngorongoro  septemba 24, 2013.
Vijana wa Kisonjo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji Digo Digo wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  (kushoto) akihutubia mkutano wa hadhara   katika kijiji  cha Digodigo  wilayni Ngorongoro, Septemba 24, 2013.