Tangazo

September 25, 2013

KAMPENI YA KUHAMASISHA ULAJI WA VYAKULA VYENYE VIRUTUBISHI ILIVYOFANA JIJINI DAR

 
Wakazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam, wakipata burudani huku pia wakipewa  elimu ya utumiaji  wa vyakula vilivyoongezwa Virutubishi na vijana wa kiundi la black worious wakati wa walipokuwa wakifanyakapeni ya  utumiaji wa vyakula vyenye virutubishi . Kampeni hiyo  inaongozwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania.(TFDA) katika  Wilaya za Kinondoni ,Ilala na Temeke ambapo mlaji anatakiwa kuhakikisha ananunua vyakula vilivyowekwa  nembo ya Virutubishi.
Vijana wanaohamasishaji  wa  utumiaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi wakitoa elimu hiyo katika mitaa ya Tandika Sokoni  jijini Dar es Salaam, Kampeni hiyo ya uhamasishaji juu ya kuongeza virutubishi kwenye unga wa ngano,unga wa mahindi na mafuta ya kula unazihusisha Wilaya za Kinondoni ,Ilala na Temeke ambapo mlaji anatakiwa kuhakikisha ananunua vyakula  vyenye nembo ya Virutubishi. Kampeni hiyo  inaongozwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania.(TFDA).
Wakazi wa Tandika Sokoni jijini Dar es Salaam, wakiwa wamefurika wakati  walipokuwa wakipewa elimu ya  utumiaji wa  vyakula vyenye vitutubishi katika Kampeni inayoendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania.(TFDA)  katika Wilaya za Kinondoni ,Temeke na Ilala.Mbiu ya promosheni hiyo ni kuhakikisha wananchi wanatumia vyakula vywenye nembo ya Virutubishi.

 

No comments: