Tangazo

September 16, 2013

WAREMBO WA TAJI LA MISS TANZANIA WATAKIWA KUPENDA BIDHAA ZA NDANI




Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' David Mgwassa akizungumza na waandishi wa habari baada ya warembo wanaowania taji la Miss Tanzania kufanya zihara katika Kampuni hiyo mwishoni juzi ambayo imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Zanzi  .Picha na mpiga picha wetu

Baadhi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakichukua chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi   ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu

Baadhi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi'  juzi  Konyagi  ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu

Meneja masoko  ya ndani na nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ,Vimal Vaghmaria kushoto na meneja masoko wa ksampuni hiyo Joseph Chibhee wakigonganisha grass na Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea kiwandani  juzi Konyagi ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu

Meneja masoko  ya ndani na nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ,Vimal Vaghmariakatikati akiwa katika pozi na baadi ya washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania walipotembelea kiwandani  juzi konyagi  ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi.
 Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi'  juzi konyagi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi.


Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakipata chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi'    ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi.
**************

NA MWANDISHI WETU



WAREMBO wanaowania taji la Miss Tanzania wametakiwa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.



Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries (KONYAGI) Bw. David Mgwassa wakati akiongea na Warembo 30 wanaowani taji la Miss Tanzania walipotembelea kiwanda hicho jijini Dar es salaam.



"Nyinyi ni mabalozi wazuri wa kutangaza bidhaa za humu ndani  hivyo nawaomba sana mzipende na kuthamini sana bidhaa zote zinazozalishwa na viwanda vya ndani" alisema Bw. Mgwassa.



Amesema kuwa TDL kupitia kinywaji cha Zanzi imeamua kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa kiasi cha Milioni 40 ikiwa na lengo la kutangaza kinywaji hicho na pia kuboresha shindano hilo.



Kwa mujibu wa Bw. Mgwassa shindano la Miss Tanzania ni kielelezo muhimu kwa taifa hili na kuwataka warembo hao kutangaza milima kilimanjaro na pia kuitangaza Zanzi kuwa ni bidhaa bora kwa Watanzania kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.



"Nyinyi warembo naombeni sana  Zanzi iwe kwenye mawazo yenu kila siku na muitangaze Zanzi baada ya mlima kilimanjaro kwa kufanya hivyo basi uchumi wa nchiu pia utakua mzuri zaidi." alisema



Kwa upande wake meneja masoko wa TDL, Bw. Vimal Vaghmaria aliwataka warembo hao kuwa na nidhamu kubwa wanapokuwa kambini kwa lengo la kupata mrembo mwenye viwango vya juu na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.



"Sisi kama TDL kupitia kinywaji cha Zanzi tumemua kudhamini shindano hili la Miss Tanzania tukiamini kuwa nyinyi ni mabalozi wazuri wa kuitangaza kinywaji hichi na kuiletea sifa Tanzania" alisema Bw. Vaghmaria.



Katika ziara hiyo warembo walipata nafasi ya kujione shughuli mbalimbali za kiwanda hicho kuanzia mwanzo wa vinywaji vinapozalishwa hadi kwenye sehemu ya mwisho ya upakiaji.

No comments: