Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya |
• Wateja wanaweza kuamisha
pesa kutok kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti ya Airtel money
masaa 24 siku 7 za wiki.
• Ni njia salama, rahisi ya
kupata pesa kupitia kutoka Airtel
Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel
money imeanzisha ushirikiano na benki mbalimbali nchini na kuwawezesha wateja
wake kuhamisha pesa kutoka kwenye benki akaunti zao na kuziweka kwenye akaunti
ya Airtel money
Banki ambazo zimeingia katika ushirikiano huo na
Airtel ni pamoja na Tanzania Postal Bank, Bank of Africa, Kenya Commercial
Bank, Barclays Bank, Akiba Commercial Bank, Exim Bank, Amana Bank, Mkombozi Commercial Bank na Standard Chartered bank.
Akiongea juu ya ushirikiano huo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya alisema” kuanzishwa kwa mpango
huu wa huduma ya Airtel money na za kibenki kutawawezesha wateja Airtel kutoa
pesa kwenye akaunti zao za benki na kuziweka kwenye simu zao yani akaunti ya
Airtel money kirahisi bila kutembelea ofisi za benki.
Huduma ya Airtel
Money ni suluhisho la huduma za kifedha ikiwa na zaidi ya mawakala 20,000 ,
kupitia mtandao wetu mpana ulioeneea nchi nzima tunauhakika wa kuwafikia
watu engi zaidi hasa wa maeneo ya
vijijini”
Tunaamini ushirikiano na benki zingine
kutaendelea kuwaletea wateja wa huduma ya Airtel money ufanisi na urahisi wa
upatikanaji wa fedha kutoka kwenye benki zao wakati wote mahali popote nchi
nzima.”
Mallya aliendelea kusema Airtel imedhamiria
kutoa huduma za kiubunifu kwa watanzania kwani tunatambua tecknologia ya simu
inazidi kukua na kuunganisha watu na kubadili maisha ya jamii.
Huduma ya
Airtel money inatoa mwanya kwa
makampuni, watoaji huduma za kitechnologia inawezesha huduma za malipo na
kukuza huduma za kifedha nchini. Airtel imejipanga kutoa huduma za kifedha na
kuiwezesha kuwa ya mafanikio aliongeza Mallya.
Akiongea kuhusu ushirikiano meneja huduma wa
Airtel Money Bw , Asupya Nalingingwa Alisema”
unafuraha kuingia kwenye makubaliano haya ya ushirikiano wa kutoa huduma
za kifedha na benki hizi tofauti ambapo kwetu ni nafasi nzuri ya kuendelea
kuboresha huduma za kifedha nchini na kuwafikia wateja wa benk hizi na wateja wa
Airtel wasio na huduma ya benki hizo maeneo ya karibu.
Ili kupata orodha ya huduma za benki husika
mteja anatakiwa kupiga namba zifuatazo na kufuata maelezo Tanzania Postal Bank
–*150*21#, Bank of Africa –*150*13#, Kenya Commercial Bank –*150*22#, Barclays
Bank –*150*20#, Akiba Commercial Bank –*150*10#,
Exim Bank –*150*11#, Amana Bank –*150*12#, Mkombozi Commercial Bank –*150*06# ,
Standard Chartered Bank – *150*65#
Huduma ya Airtel money inawawezesha wateja
kulipia bili zao, kutuma na kupokea pesa na kufanya miamala mbalimbali, huduma
hii inapatikana kwa wateja wa malipo ya awali na ya kabla , kujiunga na huduma
hii ni bure kwa kupita maduka ya Airtel na mawakala nchi nzima. Mpaka
sasa Airtel Money inamawakala zaidi ya 20,000 Wanaotoa huduma za kifedha
kwa wateja nchini. Airtel inatoa huduma ya Airtel money kwa msharika na watu
binafsi kama njia mbadala ya malipo.
Airtel pia kupitia Airtel Money kwa sasa
imezindua promosheni mpya ya Hakatwi mtu hapa nayowawezesha wateja wa Airtel
kutuma na kutoa pesa bila makato yoyote popote pale nchini.
No comments:
Post a Comment