• Vifurushi vya yatosha vyaongezwa muda
wa kupiga mitandao yote dk 61, GB 1.5 na sms bila kikomo
Dar es Salaam
October 15, 2013 Mshindi wa nyumba ya tatu ya Airtel Yatosha, Bi. Husnat
Anthony leo amekabidhiwa rasmi cheti chake cha ushindi ikiwa ni uthibitisho
maalum wa ushindi wake .
Mshindi huyo anakuwa ni mshindi wa tatu kuibuka na nyumba kupitia promosheni ya
Airtel yatosha shinda nyumba tatu baada ya nyumba ya kwanza na ya pili
kuchukuliwa na Sylvanus Juma pamoja na Agnes Lyimo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa cheti chake, Bi. Husnat alisema
“Kweli sikutegemea kama ipo siku naweza nikamiliki nyumba yangu mwenyewe, na
hata nilipopigiwa simu sikuamini ila Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuwa
mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha”
“Pia nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na nimeamini kweli Airtel yatosha
na inasaidia kupunguza makali ya maisha kwa watanzania,” alisisitiza Bi.
Husnat.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema Airtel
inayo furaha kumpata mshindi mwingine wa nyumba na haitoacha kutoa huduma bora
na zenye manufaa kwa wateja wake nchi nzima na kwa sababu hiyo bado inazidi
kuboresha huduma zake na kuzifanya ziwe za kisasa zaidi.
“Airtel hatujaishia tu kwenye utoaji wa nyumba bado tunaendelea kuboresha
huduma zetu na kuhakikisha wateja wetu wananufaika zaidi na huduma tunazotoa”
Alisema Mmbando.
Airtel imeboresha zaidi huduma zake na sasa hivi ukijiunga na kifurushi cha
siku cha 999 unaweza kupata dakika 61, kutuma ujmbe mfupi wa maneno bila kikomo
pamoja na 1.5GB kwa ajili ya matumizi ya Internet.
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel mteja anapaswa kupiga *149*99#
na uchagua 1 au 2 kisha aweze kujiunga
na kifurushi chochote cha Wiki, Siku au Mwenzi.
Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha imetoa zawadi ya pesa taslimu
shilingi milioni 90 kwa wateja wake na nyumba tatu zenye thamani ya milioni 65
kwa kila moja tayari zilishapata washindi.
No comments:
Post a Comment