Tangazo

September 12, 2011

Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma SOCIOLOGY CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) yatoa salam za Rambirambi

 UDOMSSO
Kwa niaba ya Jumuiya ya Wanafunzi Wanaosoma Shahada Ya Kwanza Ya Sosholojia (Bachelor Of Arts in Sociology) ya Chuo Kikuu Cha Dodoma   inapenda kuwapa pole watanzania wenzetu wa Tanzania Bara Na Visiwani Zanzibar kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa
 
Wanafunzi tunaosoma Shahada ya Kwanza Chuo Kikuu Cha Dodoma Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambi Rambi Kwa Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete na Raisi Wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Kufuatia Msiba Mkubwa uliolikumba Taifa.

Baada Ya Kuzama Kwa Meli Ya Spice Ireland Usiku Wa Kuamkia Jumapili ambapo Mamia ya Watu waliweza Kupoteza maisha na Wengine Kujeruhiwa Na Wengiwe wakiwa hawajurikani wapi walipo mpaka sasa.

Vilevile Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambirambi Kwa Ndugu, Jamaa Na Marafiki ambao wamepoteza Jamaa,Ndugu, Marafiki zao Katika Ajali hiyo Kubwa iliyoikumba Taifa letu

Pia tunatoa Salamu zetu Za Rambi Rambi Kwa Mwanafunzi Mwenzetu LAHYA Na Wengine Wote Walioguswa moja kwa moja Na Ajali Hii ya Meli iliyopelekea Kupoteza maisha ya Watu wengi.

Wanafunzi Wote Tunaosoma Shahada ya Kwanza Ya Sociology na Shahada Nyingine Za Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) tunaungana na Taifa kwa pamoja katika wakati huu mgumu na pia tuko tayari kushirikiana kwa hali na mali kuwafariji ndugu na jamaa kwenye msiba huu.
 
Mungu azilaze Roho Za Marehemu Mahala Pepa Peponi Amina na Mungu Awabariki Na Kuwajaza Nguvu Ndugu, Jamaa na Marafiki Kwa Kuwapoteza Wapendwa Wao
 
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

 Imetolewa na: 
Josephat Lukaza 
AFISA UHUSIANO  
THE UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION(UDOMSSO).

No comments: