Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Soka ya Villa Squad Fc ya Magomeni Kinondoni, Jijni Dar es Salaam inayoshiriki
michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), imewaangukia
wadau wa soka kuwapaga tafu ili kuweza kurejea ligi kuu Tanzania Bara.
Akizungumza Mweka hazina wa Villa, Alwan Geyash alisema kuwa hadi sasa klabu hiyo inaukata mkubwa
hali inayopelekea kuvunjika nguvu hata hivyo wanawaomba wadau kujitokeza na
kuichangia kufikia malengo yake kwani wanaamini ikiwezeshwa itaweza kurejea
ligu kuu.
“Timu ina uwezo na molali wa kutosha, lakini mifuko
imekauka kiasi tunachopata cha
kuchangishana viongozi wenyewe kwa
wenyewe ni kidogo, tunaomba wadau wa soka kujitokeza na kutuchangia kuongeza nguvu
zaidi ya kufanya vizuri” alisema Alwan.
Na kuongeza kuwa, kwa
wadau watakao guswa wanaweza kufika katika klabu hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa
Kionga ama kuchangia kupitia
akaunti ya benki ya DTB namba 0704757001
(villa squad football club)au kupitia
tigo pesa 065269999 kwa jina la mweka hazina wa klabu hiyo.
Alwan pia alisema kwa wadau wenye vitu vya kuchangia
wanakaribishwa ikiwemo vifaa vya mazoezi, maji ya kunywa,madawa ya michezo na
pesa kwa ajili ya posho za wachezaji
ambapo wanaweza kufika kwenye mazoezi
wanakofanyia uwanja wa Garden Kinondon.
Aidha, kwa upande wake Katibu Mkuu wa Villa, Mbarouk Kassanda
alisema watahakikisha wanajituma kurejea ligi kuu ya Tanzania Bara msimu
ujao licha ya kuwa kwenye kundi la kifo.
“Tumefikisha pointi saba na tupo nafasi ya nne, tunahakika
kupanda hadi kileleni tutakapofanya
vizuri kweye michezo yetu iliyobaki” alisema Kassanda.
Villa ipo kundi B, ikiwa na timu za Ndanda (Mtwara), African Lyon, Friends Rangers, Green Warriors
, Polisi DSM, Tessema na Transit Camp
zote za Dar es Salaam.
Ligi hiyo yenye kushirikisha jumla ya timu 24, iliyo kwenye
makundi matatui huku kwa kila kundi ikitakiwa kutoa timu moja kupanda ligi kuu.
Makundi mengine ni
kwa kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale
(Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma),
Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).
Kwa upande wa kundi
la mwisho C, lina timu za JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui
(Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora),
Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).
No comments:
Post a Comment