Tangazo

November 5, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA KOROSHO NCHINI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza na baadhi ya wadau wa Sekta ya Korosho, wakati akiagana nao baada ya kufungua rasmi Kongamano la Sekta ya Korosho Nchini. Kongamano hilo lililofunguliwa limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Mudhihir Mudhihir. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Kongamano la Wawekezaji wa Sekta ya Korosho nchini, lililofanyika jijini Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere. Picha na OMR
Waziri wa Kilimo, Eng. Christopher Chiza, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Mudhihir Mudhihir, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Kilimo, kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua kongamano hilo.
Makamu wa Rais Dkt.Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria Kongamano hilo,baada ya ufunguzi. Picha na OMR
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.

No comments: