Tangazo

November 6, 2013

PROIN PROMOTIONS YAJA NA MFUMO MPYA WA UUZAJI FILAMU ZAKE

Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evans Stephen (kushoto) akionyesha aina ya makabati ambayo yataanza kupatikana katika Saloon zote maarufu Hapa Nchini Tanzania ambazo zitakuwa na filamu kutoka Proin Promotions tu, filamu ambazo zitauzwa katika Saloon hizo ambapo wateja wanaofika katika saloon hizo wanaweza kujinunulia filamu hizo bila kupata usumbufu wowote ule. Kulia ni Afisa Mipango na Mauzo wa Proin Promotions Limited Abraham Lesulie.

Na Josephat Lukaza
Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Utengenezaji, uuzaji na Usambazaji wa filamu za kitanzania ya Proin Promotions limited imekuja na staili mpya ya uuzaji wa filamu zake nchini, Staili hiyo ya uuzaji wa filamu zake umekuja baada ya kugundua kuwa watanzania wengi wanakosa nafasi ya kuweza kununua filamu za kitanzania kutoka na kuwa sehemu za uuzaji kuwa chache na mbali, kutokana na tatizo hilo kampuni hiyo hiyo ikaumiza kichwa na kuja na staili hii ya uuzaji ambapo kutakuwa na makatabi ya filamu ambayo yatapatikana katika saloon zote maarufu nchini Tanzania ambapo zitakuwa na filamu za proin promotions tu ambapo mwenye saloon atanunua filamu hizo za proin promotions na kupewa kabati hilo na kuwarahisishia wateja wanaofika katika saloon zao kuweza kununua filamu hizo na kuwafanya wasihangaike katika kutafuta filamu za kitanzania
Kwa mara nyingi tena Proin Promotion imeweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu nchini kwa kuanza Proin Promotions imeanza na uuzaji wa Filamu ya kwanza na ya pili (Part 1 na Part 2) kupatikana katika Kasha Moja hii ni ya kwanza kabisa kutoka Proin Promotions Limited na bad Proin inakuletea vitu vizuri.
Jinsi ya Kuweza kupata kabati la Proin Promotions kwaajili ya kuweka filamu zake na kuweza kuuza wasiliana nao kupitia ukurasa wao wa faceebook unaopatikana kwa kiunganishi hiki https://www.facebook.com/proinpromotions au kutembelea tovuti yao ya http://www.proinpromotions.com au kwa simu namba 0712512944.

No comments: