Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi,
Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa
mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar. (Picha na Francis
Dande)
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi,
Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa
mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar.
Na
Francis Dande
WARATIBU
wa Tamasha la Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions ya Jijini Dar es Salaam,
kwa mara ya kwanza wamesema kuwa watapeleka uhondo wa tamasha hilo katika mji
wa Zanzibar.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa
kutikisa kwa mara ya kwanza katika mji wa Zanzibar, Alex Msama alisema kuwa
mbali ya Zanzibar, mkoa mwingine ambao umeongezeka ni Tanga.
Msama
aliwataka wakazi wa Zanzibar na vitongoji vyake kuunga mkono kwa kujitokeza kwa
wingi katika Tamasha, hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa Mao
Tse Tung, ambapo sehemu ya fedha zitapelekwa katika kusaidia kuwalipia ada
watoto yatima wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Hivyo,
Msama aliwataka Wazanzibar kufika kwa wingi katika tamasha hilo ili kufanikisha
malengo hayo, kama alivosisitiza kwa wakasi wa mikoa yote ambayo tamasha hilo
litarindima.
Katika
kufanikisha mpango huo, Msama ambaye ni Mkurugenzi pia wa Msama Promotions,
ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki, wadau na wapendwa katika Kristo Yesu,
wajitahidi kumuunga mkono kwa kufika kwenye Tamasha hilo litakalozinduliwa
rasmi Desemba 25 jijini Dar es Salaa, kisha kufanyika katika mikoa saba.
Alisema baada ya Dar es Salaam, litahamia mkoani Morogoro
Desema 26 kabla ya kwenda Moshi, Desemba 28 kisha kuvamia jiji la Arusha
Desemba 29, na mjini Dodoma,
mikoa mingine ni Tabora, Tanga, Mbeya na Mwanza.
Alisema mbali ya malengo mengine, pia tamasha la hilo litakuwa
na ujumbe wa kuhimiza amani nchini chini ya kaulimbiu ya ‘Tuilinde na
Kuidumisha Amani Yetu.’
Kwa
upande wa waimbaji watakaopamba tamasha hilo la kimataifa, ni kutoka Afrika
Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na wenyeji
Tanzania.
Msama
alisema kuwa maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yanakwenda
vizuri na kuwataka watu wajitoleze kwa wingi kupata ujumbe wa Neno la Mungu kwa
njia ya sauti za waimbaji mahiri waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia
hiyo.
No comments:
Post a Comment