Tangazo

September 7, 2014

JESHI LA POLISI MKOANI GEITA ZAKAMATA BUNDUKI SABA ZILIZOPORWA KITUO CHA POLISI , MTU MMOJA ATIWA MBARONI

Habari zilizopatikana leo zinasema Jeshi la Polisi mkoani  Geita limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu kadhaa ya machozi eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe ikisadikiwa kuwa ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  jana. Bunduki hizo, nne zikiwa SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuri la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinapasha pia kwamba katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi hilo pia limemkamata mtu mmoja anayehisiwa kuwa ni  jambazi  akiwa na bomu  juu ya mti, na kwamba mtu huyo ambaye hakufahamika jina alikutwa juu ya mti majira ya jioni ya leo. 

Jeshi la polisi nchini tayari limetangaza dau  la shilingi millioni 10 kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kuwakamata au kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo. Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea kwa kadri zitavyopatikana.

No comments: