Tangazo

September 8, 2014

Serikali yajipanga kutafuta suluhu ya tatizo la uharibifu wa tabaka la ozini Tanzania

Mkurugenzi  wa Mazingira Ofisi ya  Makamu wa Rais Dk. Julius Ningu  akizungumzia uharibifu wa Tabaka la Ozoni  utokanao na matumizi ya gesi  zisizo rafiki kwa Mazingira, Ofisini kwake leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Saalam.
Mkurugenzi  Msaidizi  Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Magladena Mtengu,  akitoa  ufanunuzi kuhusu mikakati inayo chukuliwa na Serikali katika kuelimisha umma juu ya uharibifu wa Tabaka la Ozoni  inayosababishwa  na matumizi ya gesi hatarishi  kwa Mazingira  akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Saalam leo.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Serikali kwa kupitia mkataba wa Motrial wa mwaka 1987  imejipanga thabiti katika kuhakikisha kuwa tatizo la uharibifu wa tabaka la ozini linapata suluhu Tanzania.

Mkurugenzi wa Manzingira Ofisi ya Makam wa Rais, Dk. Julius Ningu aliyasema hayo ofisini kwake katika maojiano na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya hatua ya serikali katika kudhibiti uharibifu wa tabaka la Ozoni.

Dk. Ningu alisema kuwa kabla ya mwaka 1985 wanasayansi waligundua kumomonyoka kwa tabaka la Ozoni, umomonyokaji huo ulipelekea wanasayansi  kutoa mapendekezo  kwenye umoja wa mataifa, na umoja wa mataifa wakaamua kuitisha  mkutano wa nchi wanachama mwaka 1985 na mkutano ulifanyika Vienna-Australia ambako ndiko uliko anza mkataba  wa Vienna wenye lengo la kusitisha uzalishaji wa gesi zinazo momonyooa tabaka la Ozoni.

Sanjari nahayo alisema kuwa Serikali imejipanga vyema katika kuakikisha kuwa inatoa elimu kwa Umma juu ya swala la gesi ambazo sirafiki kwa mazingira na  aliaainisha kuwa mpaka sasa wataalamu wapatao 400 walipatiwa mafunzo ya jinsi ya kugundua gesi zisizo rafiki pamoja na kuweza kutambua na kufichua watu wanao tumia gesi hatarishi.

Akibainisha baadhi ya vifaa vyenye mchanganyiko wa gesi hatarishi Dk. Ningu alisema kuwa air fresh,  rangi za kupaka kwenye nyumba na magari, viyoyozi mitumba, majokofu mitumba na madawa ya kuulia wadudu mashambani na manyumbani nyingi zinachakachuliwa na kuwa na kemikali hizo hatarishi.

Katika kubainisha madhara ya uharibifu wa tabaka la Ozoni DK. Ningu alisema kuwa yapo madhara mengi na makubwa yatokanayo na uharibifu wa tabaka la Ozoni kwa viumbe hai na mimea, alibainisha  madhara hayo ni kama vile saratani ya ngozi, utindio wa ubongo, na mtoto wajicho.

Kwa upande wake Mkurungezi msaidizi wa Idara ya Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Magdalena Mtengu alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na taasi mbali mbali imefanikiwa kutoa elimu juu ya swala zima la matumizi ya gesi rafiki kwa tabaka la Ozoni, aidha alisema kuwa mpaka sasa tayari mpango huo umesha ingia kwenye baadhi ya vyuo vya ufundi kama vile Veta Changombe Dar es salaam, Veta Moshi, Chuo cha Uvuvi Nyegezi Mwanza, Chuo cha ufundi Arusha, Dar es salaam Institute  of Technology,  Taasisi ya Sayansi na Technology Karume Zanzibar, Chuo Kikuu cha Sayansi na Technology  Mbeya, Veta JKT, Veta YMCA, Kihonda Morogoro, Taasisi ya Taafa ya Usafirishaji, na Taasisi ya Uvuvi Bagamoyo.

Katika kupambana na uharibifu wa tabaka la Ozoni serikali imekumbana na  changa moto mbali mbali kama vile ufahamu mdogo wa wafanya biashara wetu juu ya gesi rafiki  na zisizo rafiki kwa tabaka la Ozoni, suala la uelewa mdogo wa wanachi juu ya gesi hatarishi kwa matumizi.


No comments: