Kutokana na habari za
mara kwa mara katika vyombo vya habari nchini Tanzania, Ubalozi wa Shirikisho
la Jamhuri ya Ujerumani unatamka: Serikali ya Ujerumani kimaadili haiingilii
mambo ya siasa za ndani za nchi zingine.
Kutokana na hali hii,
Serikali ya Ujerumani na maafisa wake hawafanyi ushawishi wowote kuhusu
mwelekeo wa mjadala wa katiba unaoendelea hivi sasa nchini Tanzania.
Mashirika mengi ya
Kijerumani yanafanya kazi na mawakala wa asasi za kiraia duniani kote
kuimarisha shughuli za mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Aina hii ya
ushirikiano hufanyika pia nchini Tanzania. Shughuli hizi hulenga hasa katika
mipango ya elimu na mafunzo.
Utaratibu wa mipango hii hutolewa kwa wawakilishi wa vyama vyote vikubwa vya
siasa nchini Tanzania.
Shughuli za kisiasa
huwa hazisaidiwi au kufadhiliwa na mashirika haya, ambayo
hutenda kazi zake kwa kutumia pesa zinazotolewa na Serikali ya Ujerumani.
hutenda kazi zake kwa kutumia pesa zinazotolewa na Serikali ya Ujerumani.
Imetolewa na:
John Merikion,
Afisa Habari
Email:
pr-100@dare.auswaertiges-amt.de,
Tel. 022 2117409
No comments:
Post a Comment