Tangazo

October 9, 2014

AIRTEL YAZINDUA DILI KWA WASANII WOTE KUPITIA AIRTEL TRACE MUSIC STARS

Meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando akizindua na kutangaza rasmi  namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa kukerekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana
Balozi wa airtel music stars Tanzania Ommy Dimpos akitangaza rasmi  namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa kukerekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana Coco beach.
Mmoja kati ya wasanii  waliojitokeza  akijaribu kuimba kwenye namba maalum ya kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Stars katika viwanja vya coco beach huku meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando akishuhudia. Airtel imezindua mashindano haya ya Airtel Trace Music stars kwa lengo la kuwasaidia wasanii wanaochipukia nao kufikia malengo yao.
Baadhi ya  wasanii waliojitokeza wakijaribu kuimba na kurekodi kwenye namba maalum ya kushiriki mashindano ya airtel trace music stars katika viwanja vya coco beach ambapo airtel ilimezindua rasmi namba ya kushirmaki shindano la airtel trace music stars kwa lengo la kuwasaidia wasanii wanaochipukia nao kufikia malengo yao ya kuwa nyota wa muziki.
Wasanii wa kundi la Yamoto band wakiwa na msanii maarufu nchini ambae pia ni balazo wa airtel trace music stars tanzania Ommy Dimpos wakionyesha namba maalum itakayotumika kupiga na kutuma nyimbo kwa wasanii chipukizi kwenye shindano la airtel trace music stars lililozinduliwa rasmi jana.
Msanii wa kundi maarufu na linalofanya vizuri toka TMK Yamoto band akionyesha vitu vyake. 
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

* Piga simu namba 0901002233 Imba na Ushinde na Airtel Trace Music Stars

KAMPUNI ya simu za mkononi ya airtel imezindua rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya Airtel Trace Music Stars kwa kurekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi huku baadhi ya wasanii chipukizi wakipata nafasi yakuonyesha vipaji vyao katika viwanja vya Coco Beach.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliopambwa na burudani mbalimbali ikiwemo Yamoto bendi katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando amesema kila mtanzania anayo nafasi ya kushiriki  katika shindano hilo kwa kupiga
simu namba 0901002233.

Aidha Mmbando ameongeza kuwa lengo la kuanzisha shindano hilo ni kuinua vipaji vya watanzania wenye kujua kuimba ili wapate nafasi ya kuwa staa wa kimataifa.


Nae balozi wa shindano hilo Ommy Dimpoz amewaomba watanzania kujitokeze kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo  ambapo mshindi atajinyakulia zawadi kabambe  ikiwemo kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na safari ya kwenda nchini marekani kwa ajili ya kupata mafunzo ya kimuziki na nguli wa muziki wa Amerika  Akon.

No comments: