Tangazo

November 29, 2014

MKURUGENZI MSAIDIZI WIZARA YA HABARI DKT. KISSUI S. KISSUI AFUNGUA KONGAMANO LA ULINGO WA MAENDELEO YA BIASHARA NA UCHUMI KARAKANA YA WAJASILIAMALI-WAZO HILL TEGETA

Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Utamaduni, Michezo, Habari na Vijana Dkt. Kissui S. Kissui akifungua Rasmi Kongamano la Ulingo wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi Karakana ya wajasiliamali uliofanyika Wazo Hill Tegeta, Katika Hotuba yake aliwapongeza PSPF kwa kujitoa kuwasaidia wajasiliamali kuwekeza kupitia Fao lao la Ujasiliamali na Kujiunga katika mfuko wa uchangiaji wa Hiari wa PSS, Pia aliwapongeza Haiba Foundation kwa kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo na Mwisho alitoa somo maalum kwa ajili ya kuwasaidia wajasiliamali jinsi ya kupata Kipato na kujua matumizi mazuri ya Fedha.
 Afisa Masoko kutoka PSPF Eliachi Remmy akitoa maelezo ya Kina juu ya Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS ambapo alisema kuwa mfuko huu ni Ruhusa kuwa mwanachama ukiwa raia au asiye raia wa Tanzania na anayefanya kazi nje au ndani ya nchi pia kujiunga katika mfuko huu wa PSS ni Bure kabisa. Aliongeza kuwa kama Mjasiliamali mfuko huu ni muhimu kwake kwa kuwa anaweza kulipia kirahisi kabisa hata kupitia mitandao yote ya simu. Pia alizungumzia kwa kina Mafai mbalimbali yanayopatikana PSPF kupitia Mpango wa Hiari ikiwa ni pamoja Fao la Elimu, Fao la Ujasiliamali,Fao la Uzeeni, Fao la kifo na Fao la Ugonjwa/ Ulemavu Mwisho aliwasisitiza wajasiliamali kujuinga na mfuko huo wa PSS na kuwaeleza juu ya Mkopo wa Nyumba.
 Afisa Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Michael Leon Kazimili akizungumza kwa kina Faida za Kuwekeza PSS pia alitoa tofauti kati ya Kuwekeza PSPF na katika mabenki na kusisitiza kuwa kuna faida kubwa kama mtu akiwekeza katika Mifuko ya Jamii hasa PSPF kwamba kuna faida kubwa ya asilimia 6% kama ukiwekeza PSPF, Pia alizungumzia mkopo wa nyumba ambapo alisema kwamba Mwanachama wa PSPF awe ni wa Kuchangia kwa Lazima au kwa Hiari atapata Mkopo wa Nyumba na atalipia kwa muda wa Miaka 25 kwa kuzingatia Taratibu za Mfuko.
 Mwenyekiti wa  Karakana ya Haiba Foundation Mzee Adam Kaira akitoa utangulizi kwa wajasiliamali ambapo alitoa mwelekeo wa Haiba Foundation pia alieleza kuwa kuna mpango wa kuanzisha Benki ambayo itawasaidia wajasiliamali aliongeza kuwa mpaka sasa Haiba Foudation imefanikiwa kuwa na vikundi 75 ambavyo vinafanya vizuri, Pia aliongezea kuwa wajasiliamali wanaweza kupata Mkopo kuanzia Tsh 400,000 hadi 1,000,000 na kuna wanachama walishapata, mwisho alizungumzia juu ya wajasiliamali kuwekeza katika Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS ambapo utawasaidia zaidi katika kuboresha maisha yake.
 Mkurugenzi wa Haiba Foundation Adam Ngamage akitoa mada juu ya Haiba ya Ujasiliamali ambapo alisisitiza Jinsi gani Mjasiliamali anaweza kubadili mwenendo wake wa kuwa mfanyabiashara mzuri na mbinu mbali mbali za kufanya Biashara yake iweze kwenda mbele bila kukwama Mwisho alizungumzia umuhimu wa kuwekeza kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF
 Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga-Kuku Gren Mushi Maarufu kwa Mama Kuku akizungumzia ujasiliamali lakini hasa huu wa ufugaji wa Kuku ambapo yeye ni mzoefu wa muda mrefu na ameanza tangu miaka ya 1970, alizungumzia jinsi gani wajasiliamali ambavyo wanaweza kusaidiana katika njia mbalimbali, aliongeza amesisitiza Biashara ya kuku sasa inakuwa sana na amesema kuna mpango wa kuanzisha Jokofu ya kuuzia kuku ambayo yatakuwa katika maeneo mbalimbali yakiuza kuku kwa vipande ili kila mwananchi anayehitaji kuku apate kitoweo hicho. Mwisho aliwashukuru kwa Dhati PSPF kwa moyo wao wa Dhati
 Muwezeshaji wa Kongamano hilo  kutoka Haiba Foundation Chonya Libe akiendelea kutoa Mwongozo .
 Afisa Masoko kutoka Mfuko wa PSPF David M. Mgaka akiwagawia Fomu za Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS wajasiliamali wote waliofika katika Kongamano hilo.
 
Maafisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakifuatilia kwa makini Kongamano hilo la Wajasiliamali
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa Makini Kongamano hilo
 


 Washiriki ambao ni wajasiliamali katika mambo Mbalimbali wakiwepo wauza Ubuyu, Karumati, Mkaa, Kuku, Magenge ya Mboga, Matunda, Maziwa, Chips, Mgahawa, na mengine mbali mbali wakiwa wanafuatilia kwa Makini Kongamano la Ulingo wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi Karakana ya Wajasiliamali  Wazo Hill Tegeta 
 Baadhi ya Washiriki wakijiunga na Mfuko wa kuchangia kwa Hiari wa PSS.

No comments: