Helkopta hiyo ilivyo haribika.
|
Wananchi wakiwa eneo la tukio. Kwa Hisani ya Father Kidevu |
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
HELKOPTA
ya wizaya ya Maliasili na Utalii iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya
Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani
Bw. Warren Buffet na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii
June 14, 2014 jijini Dar es Salaam imepata ajali na kuua watu wanne hii leo.
Helkopta
aina ya Robertson R44 hiyo
ambayo baade ilikabidhiwa kwa Mamlaka ya Hifadhi za Wanyamapori Tanzania
(TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya kupata hitlafu katika
injili yake.
Mashuhuda
walioshuhudia ajali hiyo eneo la Kipunguni B- Ukonga Moshi Bar Ilala Dar es
Salaam waliambia Father Kidevu Blog kuwa awali waliona helkota hiyo ikiyumba na
kutoa mngurumo usio wa kawaida na baade kuzima kisha kusikika kuwashwa bila
mafaniko na baade kuanguka.
"Tulisikia
mlio wa Helkopta usio wa kawaida, na baadae ulizima na kusikika tena kuwashwa
ikagoma lakini tukasikia tu kishindo kikubwa cha Helkopta hiyo kuanguka,"
alisema shuhuda huyo.
Kamanda
wa Polisi Viwanja vya Ndege, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Seleman
aliambia Father Kidevu Blog kuwa walio kufa ni Marubani wa tatu kati yao wawili
ni marubani wa polisi na Afisa mmoja wa Polisi.
ACP
Selemani aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai
Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba, Konstebo wa
Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan.
No comments:
Post a Comment