Kwa masikitiko makubwa
nawajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani amefariki dunia mchana huu katika
hospitali ya jeshi Lugalo alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Pia mwandishi mahiri wa
zamani wa habari za michezo nchini, Innocent Munyuku, naye amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo.
Hilo ni pigo kwa
waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla, maana wote wameondoka
wakati bado mchango wao ukihitajika sana.
Taarifa zaidi
tutaendelea kupeana kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za marehemu mahali
pema peponi.
Amina.
Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
19/11/2014
No comments:
Post a Comment