Tangazo

December 1, 2014

DK.BILAL KUWEKA JIWE LA MSINGI CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (pichani) Desemba 2 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Kijijini Kiromo,Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam Ofisa Habari wa (UB), Happiness Katabazi alisema sherehe hizo zitafanyika Kijijini Kilomo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao utaanza mapema Januari Mwaka 2015.

Katabazi alisema Dk. Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo ilikuwa ukikaliwa na watumwa.

" Sasa sisi UB tunaitambua hiyo historia na ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la Bagamoyo.Na kwakuwa kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, basi sasa kupitia UB ambayo inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote watakuwa huru kwasababu tutapata elimu" alisema Katabazi.

Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni ,Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu.

Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo. UB ilianzishwa rasmi Mwaka 2011.

No comments: