Wanafunzi
wa shule ya sekondari kiteto wakionyesha vitabu baada ya kukabithiwa na
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wake wa Airtel
shule yetu wenye lengo la kuchangia katika sekta ya elimu nchini.
xxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi wetu
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za
kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa
shule ya sekondari ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara.
Msaada
huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya
fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma
masomo hayo katika shuleni hiyo.
Akipokea
msaada huo Diwani wa kata ya Central wilayani Kiteto Mh Yahya
Masumbuko, amesema shule nyingi wilayani hapo zimekuwa zikikabiliwa na
changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba
kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.
“Ni
kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi
kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Kiteto hali
inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Mh
Masumbuko.
“Uhaba
wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya
sayansi pia ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa
wanafunzi wetu hapa wilayani” aliongeza Mh Masumbuko.
Aidha
Diwani huyo ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel kwa kuona umuhimu wa
kuboresha masomo ya sayansi ambayo ufaulu wake umekuwa mdogo hali
ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.
“Msaada
huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi
hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii
na hasa vitabu vya sayansi” alieleza Mh Masumbuko.
“Sisi
wa Kiteto tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wanafunzi wetu
wanajifunza masomo hayo na ndio maana hata mgao wa walimu tulioupata
tumeuelekeza katika ufundishaji wa masomo ya Sayansi. Alimalizia Mh
Masumbuko.
Kwa
upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto
wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwawezesha kupata
vitabu vitakavyowasaidia katika masomo yao.
Msaada
huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia
utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo ya
wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Airtel
shule yetu ni mpango endelevu uliodumu kwa takribani miaka 10 iliyopita
mpaka sasa zaidi ya shule za sekondari 1300 nchini zimeidika na msaada
wa vitabu chini ya mradi huu.
Tutaendelea kushirikiana na serikali chini
ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha sekta ya elimu na
kutoa kipaombele kwenye masomo ya sayansi ili kuwa na wanasayansi wengi
nchi ambao kwa sasa ni changamoto katika shule nyingi na nchi kwa ujumla
alisema Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kati Bwana Hendrick Bruno
No comments:
Post a Comment