WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kasikazi akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kasikazini
WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kasikazi akiwahutubia wananchi wa jimbo la mufindi kusini ambako anatarajia kugombea ubunge kupitia chadema.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi wetu
Mufindi
Mufindi
Wananchi
wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamelalamikia ugumu wa maisha
wanaokumbana nao kila kukicha licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa
rasilimali ya misitu pamoja na mazao ya biashara.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema
Taifa wilayani mufindi, Williamu Mungai mmoja wa wananchi hao Clement Mwachanga
alisema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya inayofanya vema kwa kuingiza
pato kubwa la taifa lakini wananchi wake wako katika wimbi kubwa la umaskini.
Mwachanga
amesema anashangaa wilaya kama ya mufindi inayoongoza kwa utoaji wa mbao nyingi
lakini cha kushangaza shule nyingi za msingi hazina madawati jambo
linalopelekea wanafunzi wengi kukaa chini.
‘’Hii
ni aibu kubwa sana kwa wilaya yetu haiwezekani wilaya inarasilimali za kutosha
lakini wananchi wake wengine wanashidwa hata kupata mlo mmoja kwa siku huku
watoto wao wakishidwa kupelekwa shule kutokana na kushidwa kulipa ada ya
kumuandikishia mtoto ”
Kwa
upande wake Williamu Mungai ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kulichukua
jimbo hilo la Mufindi Kaskazini ambalo kwa sasa linaongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamudu Mgimwa amewataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha
watoto wote wanaandikishwa shule za msinga hata kama hawana ada ya
kuandikishiwa kwa kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania
Mungai
alisema ni kila mtoto ana haki ya kupata elimu ya msingi kwa kuwa ndivyo katiba
inavyosema na kuwataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarudisha
majumba watoto kwa kisingizio cha kukosa hela ya kuwaandikishia
"Niwatake
wenyeviti wangu wa mitaa muhakikishe watoto wote wanaandikiswa na kama
kuna mwalimu atagona kumuandikisha kwa kisingizio eti hana shilingi eflu
hamsini jikusanyeni pamoja niiteni na mimi twende wote tuone kama hata
muandikisha kwa maana walishasema elimu bure sasa bure waliyosema ikuwapi"
alisema Mungai
Hata
hivyo mungai alisema imefika wakati wakuikomboa mufindi iliyoko katika wimbi la
umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuataka wanamufindi
kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maono ya mbali katika kuwalete
maendeleo na sio porojo za kila siku.
Mungai
alisema kuwa atahakikisha anazunguka vijiji vyote 72 vya wilaya ya
mufindi katika harakati zake za kujenga chama na kuweza kutambua kero za
wananchi na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua .
No comments:
Post a Comment