Tangazo

January 26, 2015

WASANII MKOANI IRINGA WAMEMTUNGIA WIMBO MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI FRANK KIBIKI

MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi ya ngoma  kwa mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake, ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea  ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa,  wasanii hao walisema wameamua kutengeneza wimbo huo kutokana na mchango mkubwa wa mwanahabari huyo, katika fani yao.

Msanii huyo Richard Kayombo  ‘One Lee’ ambaye alikabidhi wimbo kwa niaba ya wasanii wenzake alisema wimbo huo, unamtambulisha Kibiki, kama kiongozi wa kuigwa kutokana na tabia yake ya ucheshi na kujichanganya na watu.
akizungumza wakati wa kukabidhi WIMBO huo msanii  ‘One Lee’ alisema kuwa FRANK KIBIKI amekuwa akiwapa elimu vijana juu ya kujitambua na kuwasaidia jinsi gani ya kujiajili wao wenyewe na kuonyesha njia ya kutokea kimaisha na dio imekuwa sababu ya wasanii wa mkoani hapa kutunga wimbo huo. 

“Wimbo unaitwa ‘Kuwa mfano wa kuigwa’, tumempa kaka yetu kama zawadi, ili wengine waige mfano wake. 

Awali tulitamani uitwe Kibiki, lakini kwa sababu tunataka kuuza tumeamua kuuita jina hilo,”alisema One lee.

Alisema miaka miwili iliyopita, aliwahi kukutwa na jambo ambalo alihitaji msaada wa haraka, alihangaika lakini alipokutana na Kibiki ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, alisaidiwa jambo ambalo lilimfanya aanze kumuheshimu.

Alisema aliposikia kuwa Kibiki ametangaza nia, aliamua kushirikiana na wenzake ili watengeneze wimbo ambao hivi karibuni utaachiwa hewani.

‘One lee’alisena ngoma yake itamtambulisha Kibiki kama alivyo, na kwamba wameamua kumsaidia bila gharama yoyote kama sehemu ya mchango wao wakiamini ikiwa atafanikiwa kupenya na kupata nafasi hiyo, ataweza kuwaunganisha na kuwainua wasanii.
kwa upande wao wasanii wengine wa mkoani irnga walisema kuwa imefika wakati sasa iringa mjini itawaliwe na kiongozi mwenye uelewa juu ya kukuza uchumi wa mkoani na kuzingatia vipaji vya vijana kwa kuwa vijana ndio taifa la leo.

No comments: