Tangazo

February 26, 2015

TWANGA PEPETA NA FM ACADEMIA NANI ZAIDI? MARCH 28 NDANI YA ESCAPE ONE MIKOCHENI JIJINI DAR

Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu ushiriki wao katika onyesho la pamoja na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, linalotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini. Kutoka (wa pili kulia) ni Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, Rais wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma”, Nyoshi El Sadat, mwimbaji wa FM Academia, Mule Mule ‘FBI’ na Mnenguaji wa Twanga, Lilian Internet. Viingilio katika onyesho hilo ni 15,000/- kawaida na 20,000/- kwa VIP. PICHA ZOTE/JOHN BADI
Rais wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma”, Nyoshi El Sadat (kushoto), akifafanua jambo kuhusu ushiriki wao katika onyesho hilo. Kulia ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka na Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu.
Kiongozi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Luiza Mbutu (katikati), akifafanua jambo kuhusu ushiriki wao katika onyesho hilo. Kulia ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka na (kushoto) ni Rais wa FM Academia, Nyoshi El Sadat.
Wakata nyonga wa ‘Twanga Pepeta’, Lilian Internet na wenzake wakionyesha monjonjo yao mbele ya wanahabari.

No comments: