Tangazo

March 20, 2015

TANZANIA, JAPAN WATILIANA SAINI UJENZI WA KITUO CHA UFUNDI STADI ILEJE

1
Signing the grant contract, witnessed by Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, and Hon. Rosemary Senyamule, Ileje District Commissioner. Front line from the left: Mr. Mussa Otieno, District Executive Director, Mr. Simon Mwango'nda, Executire Director of the recipient organisation, Integrated Rural Development Organisation, Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan.

Na Mwandishi wetu

MKATABA wa Ujenzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi stadi katika Wilayani Ileje, Mkoani Mbeya umetiwa saini.

Mradi huo uliobuniwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene na Simon Kamiyoge umelenga kuwawezesha wakazi wa Ileje kuwa na taaluma ya ufundi na baadae kutumika kuendelea wilaya hiyo.

Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Kazuyoshi Matsunaga wa ubalozi wa Japan nchini na na Mwakilishi wa Integrated Rural Development Organisation (IRDO) Simon Kamiyoge wakishuhudiwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Janet Mbene , Mbunge wa Ileje Rosemary Staki na Mkuu wa wilaya ya hiyo Mohamed Maliyao Mwala, na Mwenyekiti wa halmashauri ya Ileje Musa J. Otieno na maofisa wengine wa wilaya hiyo.

Kaimu Balozi wa Japan Kaziyoshi alisema amefurahishwa sana kutiwa saini kwa mkataba huo kwa kuwa unamkumbusha miaka 70 iliyopita katikati ya vita kuu ya pili ya dunia ambapo Japan ilijikuta katika uharibifu mkubwa pamoja na kubomolewa kwa majengo ya shule.

Alisema katika vita hiyo Japan ilijikuta si tu hawana shule bali hakukuwa na nyumba, maji, umeme hamna chochote kile lakini sasa hivi Japan ni ya tatu kiuchumi.
2
Discussion between Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan, and Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade. From left: Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, Hon. Rosemary Senyamule, Ileje District Commissioner, Hon. Mohamed Maliyao Mwala, Chairperson of Ileje District Council, Mr. Mussa Otieno, District Executive Director, Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan.

Amesema pamoja na kuwa na uchumi mkubwa Japan haina gesi, haina dhahabu wala almasi kama ilivyo Tanzania.

Alisema siri ya maendeleo makubwa ya Japan ni elimu na wafanyakazi wenye ujuzi unaotakiwa.
Alisema kuonesha ukuaji wa ujuzi alisema kwamba kampuyni maarufu ya magari ya Toyota, kabla ya vita ilikuwa ni kampuni ya nguo . Lakini baada ya vita ilijibadilisha kuwa kampuni ya magari, na sasa ni namba moja duniani.

Alisema siri ya Toyota ni kuwa na wataalamu wenye ujuzi na kuwa na malengo ya wazi yanayoambatana na tamaa ya kufanikiwa katika malengo hayo.

Lengo la Toyota lilikuwa kushindana na viwanda vya Marekani na hivyo walinunua gari kutoka Marekani na kulivunja katika vipande 4000 na baadae mafundi wa Toyota wakaigiza vipande hivyo na kuunga gari kwa mikono yao wenyewe.
3
Speech by Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires. From left: Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires, Mr. Joseph Safe Mchome, District Land, Natural Resources and Environmental Officer, Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade.

Katika hatua za mwanzo magari yaliyotengenezwa yalikuwa mabaya sana lakini siku zilivyokwenda walitoa gari nzuri zaidi na sasa ni namba moja duniani.

Kwa sasa Toyota si tu kampuni yenye wataalamu tu lakini pia wataalamu hao hupewa motisha ya kuweza kutekeleza malengo yote.

Kaimu alisema kwamba kwa kuangalia uzoefu wa zamani wa kiutendaji , Japan inaamini ili kuendeleza ni lazima kutengeneza namna ya mradi unaohamasisha vijana na pia kuwapa utaalamu wa kuutumia na katika dhana hiyo wanatoa msaada kuijenga Ileje ijayo.
4
Shaking hands after the speech. From left: From left: Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires, Mr. Joseph Safe Mchome, District Land, Natural Resources and Environmental Officer, Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade.

Kituo hicho kinatarajiwa kuwanoa vijana kitaalamu katika masuala ya ufundi stadi ili vijana hao waweze kutekeleza ndoto zao na za eneo lao wanalotoka na taifa.

Mradi huo uliotiwa saini ni wa shilingi milioni 160.

Balozi huyo alitoa shukurani kwa timu ya watu waliofanikisha kupatikana kwa mradi huo na kusema wanaandaa vyema wakazi wa Ileje kwa maendeleo yao wenyewe.

Alisema serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kwamba Tanzania inasonga mbele katika kufunzi za wataalamu.
5
Discussion between Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan, and Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, at the planned construction site of vocational training centre. From left: Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires.
6
Gift from Ileje District. From left: Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires, Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and Trade, Hon. Rosemary Senyamule, Ileje District Commissioner.

No comments: