Tangazo

March 20, 2015

MAMA WA MITINDO ASIA IDAROUS KUPAMBA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI ZANZIBAR MACHI 22

11072283_933753296658934_392071823375109477_n

..burudani kutolewa na Baby J, Coconut na Zanzibar One Modern taarab

Na Andrew Chale wa Modewji blog

Machi 22 mwaka huu Kisiwa cha Unguja, Zanzibar kinatarajiwa kuwa na tukio moja kubwa litakalowakutanisha Wanawake mbalimbali na kusheherekea siku ya Mwanamke Dunia, ndani ya ukumbi wa Bwawani Hoteli.

Katika tukio hilo, linatarajiwa kuwa pia na shamra shamra ikiwemo za mitindo ya mavazi kutoka kwa gwiji wa mitindo Nchini, Mama Asia Idarous Khamsin atakaye onesha mavazi mbalimbali siku hiyo akiwa sambamba na Mbunifu wa mavazi wa Zanzibar, Matilda Revelian wa Matty Designs.

Sherehe hizo zimeandaliwa na kikundi cha akina mama cha Zanzibalicious Women Group, chenye maendeleo makubwa kwa sasa hapa nchini.
IMG_9704
Usiku huo utapambwa na burudani mbalimbali akiwemo mwanamuziki Baby J. Wengine ni bendi ya Coconut na Zanzibar One Modern taarab.

Aidha, Asia Idarous Khamisin amekisifia kikundi kilichoandaa halfa hiyo ya siku ya Mwanamke Duniani kwa Zanzibar, kwani ndio kwa mara ya kwanza Zanzibar wanawake na kusheherekea siku hiyo ya mwanamke duniani.

Usiku huo kiingilio kinatarajia kuwa sh. 35,000 kwa viti vya kawaida na sh 50,000 kwa upande wa V.I.P.

Aidha, kwa wadau wanaotaka tiketi wanaweza kutembelea katika maduka yaliyopo Mlandege Al Bashaer Tour, Magereza Ms Saloon, Michenzani Sas Saloon au kupitia mawasiliano ya simu ya namba: 0777418324, au 0777868766, 0715080399

No comments: