Tangazo

April 13, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AVALIA NJUGA TATIZO LA UBOVU BARABARA WILAYANI KWAKE


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

UCHUNGUZI JUU YA UBOVU WA BARABARA ZA WILAYA YA KINONDONI 13.04.2015

UTANGULIZI

Ndugu waandishi wa habari na ndugu wananchi, nimewaiteni leo, kuwaambia juu ya Agenda moja tu. Nayo ni Ubovu wa barabara.

Tangu sijaingia ofisini hapa, na baada ya kuingia ofisi hizi za umma, kila siku Napata fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali katika maeneo ya Kinondoni, nimekuwa nikisiliza jamii nzima ya Kinondoni, wengi kero yao kubwa ni ubovu wa barabara nchini lakini hasa wakiinyooshea kidole wilaya yangu ya Kinondoni. Mimi nitazungumzia ubovu huo katika wilaya yetu hii ya Kinondoni. 
Wananchi wamekuwa wakilalamika juu ubovu wa barabara, wanasema barabara zinajengwa chini ya viwango, kiasi lami inawekwa leo lakini haimalizi miezi sita inabanduka na inaacha mashimo. Kwamba mashimo yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida ya barabara zetu hapa Kinondoni. Mitaro haipitishi maji kama inavyotakikana, Mitaro mingine inachimbwa mifupi kuliko mahitaji halisi, barabara zinakuwa nyembamba kutoka kushoto kwenda kulia, pia wembamba kutoka chini ya lami hadi juu (Surface area). Kwamba ujenzi wa barabara katika Wilaya yetu hauendani na kasi ya mahitaji na kukua kwa mji. Wananchi wana ichallenge Seriklai kuwa inawezekana kasi ndogo ya kujengwa wka barabara za WIlaya inatokana na sababu kuwa kila siku tunakarabati barabara badala ya kujenga kwa ubora ili tupanuwe wigo wa huduma! Wapo wananchi wanaohoji iweje ubovu huu wa barabara uachwe hivi hivi kiasi serikali ipo na haioni kama kuna tatizo. 
Jambo hili limenistuwa, nikaona mengi ya madai haya na mengine ambayo sijayaeleza yana msingi, na nikasema si busara kuwaacha wananchi wananung’unikia hali hii ili hali wao wenyewe ndio walipa kodi wakuu. Hawa wananchi wana haki ya kujuwa thamani halisi ya fedha ambayo ni kodi yao je inalingana na gharama halisi ya miradi ya ujenzi?

DHIMA HALISI

Sasa mimi binafsi si mtaalamu wa masuala ya Uandisi wala usanifu, nikasema hili suala ni lazima tulichukulie kwa umakini na tulipatie majawabu, hivyo basi nimeunda tume huru ya wataalamu, itakayojumuisha Wasanifu, Waandisi, wataalamu wa Mikataba, wataalamu wa Ugavi na Manunuzi na watu wengine kutoka vyombo vyetu mbalimbali vya uchunguzi ili wakachunguze pamoja na mambo mengine, usanifu wa barabara zetu kama unazingatia viwango, taratibu za manunuzi na kutoa tenda kama zinazingatiwa, wakandarasi wetu wazalendo kama wanawajibika ipasavyo au kuna njama yeyote inafanywa ili kuhujumu kazi wanazopewa, je waansishi wetu wanatimiza wajibu wao ipasavyo katika mchakato mzima wa usanifu na ujenzi ili kuhaklikisah ubora wa barabara unafikiwa?

MATOKEO YA TUME

Tume hii itafanya kazi kwa siku 21 kuanzia tarehe 15.04.2015 na kukabidhi ripoti yake tarehe 5.May.2015 saa 4:00 asubuhi ofisini hapa, mbele yenu waandishi wa habari. Matokeo ya ripoti hiyo ndiyo itakayotoa majibu wa ama tupanuwe wigo wa uchunguzi mpaka kwenye kandarasi zingine za ujenzi wa shule za serikali, ofisi za umma za Wilaya au la, Majibu yatapatikana baada ya kupata taarifa hii.

Ninaamini kwa njia hii ya uwazi na ukweli majibu ya haki juu ya kilio cha wananchi yatapatikana. Ili kubaini chanzo na ukubwa wa tatizo. Majibu hayo naamini hayatamuumiza mtu isipokuwa tu kama anahusika na ubadhirifu na uzembe utakaobainika.

WAJUMBE WA TUME

1)Eng. Julius Mamilo Contractor Specialist – National Construction Council NCC - Mwenyekiti

2) Eng. Ronald Rwakatare Road Fund Department of Value for Money- Katibu

3) John Malisa – Cental Milo Laboratory - (CML)Mjumbe

4) Abednego Lyaga – Procurement Specialist – Mjumbe

5) Eng. Patrick Balozi (Engineers Registration Board) – Mjumbe

Na wajumbe wengine wawili kutoka vyombo vingine vya serikali vinavyoshughulika na uchunguzi.

Terms of Reference zimeambatinishwa kwa rejea yenu ambayo kamati itaifanyia kazi.
Imetolewa na

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Paul Makonda.

No comments: