Tangazo

April 13, 2015

'Airtel Shule Yetu' yamwaga vitabu vya sayansi katika Shule ya Sekondari ya Kutukutu mkoani Morogoro

Wanafunzi wa shule ya sekondari Handeni iliyopo wilayani Handeni wakisoma vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya Airtel shuleni hapo kwa ajili ya masomo ya sayansi vyenye thamani ya sh.milioni mbili.
Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel Kanda,Aluta Kweka (kulia) akimkabidhi aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweymamu vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na kampuni hiyo vyenye thamani ya sh.milioni mbili anayeshuhudia katikati ni Mwalikishi wa Afisa Elimu wilaya ya Handeni, Ally Mwinyuma ambaye alimuwakilisha pia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.



Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Handeni,Ally Adamu kulia akimkabidhi kitabu mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Aisha Juma cha Fizikia ambavyo vilitolewa na kampuni ya simu za mikononi nchini Airtel vyenye thamani ya sh.milioni mbili.
XXXXXXXXXXXXXXXXX
 
MOROGORO
Uongozi wa shule ya sekondari ya Kutukutu iliyopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, umeishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi.


Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni mbili umekabidhiwa hivi karibu na wawakilishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikiwa ni mpango wa SHULE YETU unaosimamiwa na kampuni hiyo.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo mkuu wa shule ya sekondari Kutukutu Finyilise Elias amesema, utasaida kuongeza ufaulu wa wanafunzi wake wanaosomea masomo ya sayansi.

Mwalimu Finyilise amesema, kumekuwa na ufaulu wa kusuasua kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne hasa kwenye masomo ya sayansi hivyo msaada huo utasaidia kuongeza ufaulu shuleni hapo.

“ Wanafunzi wetu wanaosomea michepuo ya sayansi wamekuwa na ufaulu mdogo sana na hii inatokana na ukosefu wa vitabu vya masomo hayo kwa muda mrefu sasa” alisema Mwalimu Mkuu huyo.

“msaada huu utatusukuma haraka kwenye ufaulu wa kiwango cha juu wanmasomo ya sayansi kwani mwitikio wa wanafunzi wetu ni mkubwa na tunatarajia tutapata matokeo ya haraka kutokana na msaada huu wa vitabu” aloingeza Mwalimu Finyilise.

Awali akikabidhi msaada wa vitabu hivyo, Meneja wa Airtel Mkoani Morogoro Bw. Omar Bongo amesema, hatua hiyo ni kuwawezesha wanafunzi wa shule za sekondari kupata maarifa ya masomo ya sayansi kwa vitendo.

“Sisi wa Airtel tumekuja hapa kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kupitia elimu na hasa vitabu vya kujifunzia, mkazo wetu kwa sasa ni masomo ya Sayansi na tumeleta vitabu vya kujifunzia. Alisema Bw. Bongo.

Shule hiyo ya sekondari kutukutu yenye wanafunzi zaidi ya 300 bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na vyumba vya maabara na mazingira mazuri ya kujifunzia.

No comments: