Tangazo

September 5, 2015

A+E NETWORKS(R) KURUSHA DOKUMENTARI YA OJ SIMPSON

A&E_0005
Mkuu wa vipindi channel ya A & E Networks, Racheal Job akizungumza na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice nchini Mauritius. Katikati ni Mkurugenzi wa Kanda channel ya A & E Networks, Anthea Petersen na kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins.
A&E_0038
Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins akifafanua jambo kwenye jukwaa lililowakutanisha waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika nchini Mauritius.
A&E_0045
Ebenezer Donkoh kutoka YFM Ghana akiuliza swali katika mkutano wa waandishi wa habari ulionadaliwa na MultiChoice Africa.
A&E_0033
Philip Mwaniki kutoka Nairobi, Kenya akiuliza swali kwenye jukwaa hilo lililowakutanisha waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
A&E_0041
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliohudhuria wanaohudhuria kongamano hilo linalotarajiwa kumalizika leo nchini Mauritius.
A&E_0051
Na Mwandishi Wetu

DOKUMENTARI inayomhusu mmoja wa masupastaa ambaye kadhia yake ya mauaji ilitagazwa sana OJ Simpson itarushwa na na chaneli ya uhalifu na uhunguzi ya A and E Networks Oktoba mwaka huu.

Dokumentari hiyo inatolewa katika siku ya kumbukumbu ya miaka 20 ya hukumu ya moja ya kesi iliyoandikwa sana na vyombo vya habari vya Marekani.

Doukumentari ya kwanza ya The Secret Tapes of the O.J. Case: The Untold Story (itarushwa Oktoba 6, saa 21) na O.J. Speaks: The Hidden Tapes (itakayorushwa Oktoba 13 saa 21).

Dokumentari hizo zimesheheni mambo ambayo hayajajulikana kwa watu ambayo yalizungumzwa na OJ Simpson na wengine waliohusika katika tuhuma za mauaji wakati wa shauri la jinai la la kiria.
Imeelezwa nchini Mauritius kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice kwamba dokumentari hizo ni zenye msisimko mkubwa katika msimu ujao wa A+E Networks.

Mkurugenzi wa A+E Networks wa Kanda ya Afrika, Anthea Petersen : “msimu huu A+E Networks inaringia kitu kikubwa kitakachoingia sokoni cha OJ Simpson kupitia dokumentari za uhalifu na uchunguzi ( CI).”

Petersen pia alisema kwamba hivi karibuni wamefungua ofisi ya A+E Networks’ jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Mkurugenzi huyo wa A+E Networks kanda ya Afrika amesema kwamba wanawekeza katika bara la Afrika kama chaneli bora ya burudani wakiwa na upenzi wa asilimia 50 katika robo ya kwanza.
Aidha anazungumzia ujio wa programu ya Lifetime kuanzia Oktoba 16 mwaka huu itakayokuwa hewani saa 2 na dakika 50.

Kuna programu inayokwenda kwa jina la Four Weddings SA ambayo kwa sasa ndiyo inayowika na ipo kila Ijumaa.

Pia kuna kitu kizuri ndani ya HISTORY ambayo imepata haki miliki ya kutangaza filamu isiyokuwa na skrpti ya Idris Elba: Mandela, My Dad & Me, baada ya kucheza Mandela: Long Walk to Freedom.

Pia kuna shoo ya Fifth Gear ndani ya chaneli ya HISTORY, huku wakiwa na vitu vya mvuto safi kabisa kuhusu barabara za Afrika Kusini.

Mambo mengine matamu ni kama Pawn Stars SA, ikiwa katika msimu wa pili ndani ya History ityakayoanza kuonekana mapema mwakani.

No comments: