Tangazo

September 28, 2015

DStv YAJA NA CHANELI YA MAISHA MAGIC BONGO, KWA AJILI YA WATANZANIA

D3A_5097
Mkurugenzi M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice hivi karibuni nchini Mauritius.
D3A_5116
Mkurugenzi wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus akifurahi jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Na Modewjiblog, Mauritius

Moja ya makampuni yanayoongoza katika utoaji wa vipindi vya burudani barani Afrika M-Net imesema kwamba itazindua chaneli maalumu kwa ajiri ya wakazi wa Tanzania itakayojulikana kama maisha Magic Bongo.

MAISHA MAGIC BONGO itaruka hewani kupitia chaneli 160 ya DStv kuanzia Alhamisi ya Oktoba Mosi mwaka huu na itapatikana katika vifurushi vyote vya Access, Family, Compact, Compact Plus na Premium.

Imeelezwa kuwa ingawa mambo yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya Watanzania mataifa jirani yaAfrika Mashariki ikiwamo Kenya, Uganda, Ethiopia na DRC wanaweza kuona.
Uamuzi huo wa M-Net umefanyika wakati mchakato unaendelea wa kuboresha zaidi ulaji kwa wateja wake.

Hata hivyo wamesema kwamba MAISHA MAGIC EAST ambayo kwa sasa inaruka kupitia chaneli 158 itajiimarisha zaidi katika soko la Kenya huku ikiendelea na mara moja kwa wiki kwa ajili ya soko la Uganda ndani ya Luganda.
D8A_1979
Pichani ni waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa hilo lililoandaliwa na MultiChoice Africa hivi karibuni.

MAISHA MAGIC BONGO imelenga kuhudumia soko la Tanzania likionesha vipindi vya Kiswahili kwa ajili ya kutimiza pia lengo la taasisi la kuhudumia soko kwa kuangalia makundi.
Mkurugenzi wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus amesema ingawa kwa miaka mingi wamekuwa wakitoa vipindi vyenye lugha mchanganyiko kwa sasa wamepania kutoa vipindi kwa lugha ya eneo kutokana na soko kuruhusu.

“Tumefanya mabadiliko kwa nchi za Afrika Mashariki kwa siku za karibuni. Kasi ya mabadiliko hayo yanaonesha kujali kwetu. Na tutaangalia mafanikio katika MAISHA MAGIC BONGO, kuona uwezekano wa kuendelea kutengeneza chaneli zinazokidhi mahitaji Fulani.” Amesema Erasmus.
Chaneli mpya itakuwa na matangazo ya saa sita ambayo yatarejewa mara tatu kwa siku na inatarajiwa saa za vipindi kuongezeka zaidi.

Katika chaneli hiyo kutakuwa na kipindi cha saa moja cha muziki Mzooka, ambayo itakuwa mwishoni mwa wiki majira ya jioni na itakuwa kipindi cha miziki ya karibuni kutoka Tanzania. Kitakuwa ni kipindi cha wapenzi wa hip hop na Bongo.
D3B_8767
Mkurugenzi M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Movie Stars wa nchini Nigeria, Rita Dominic na Desmond Elliot mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.

Pia kutakuwa na michezo ya kuigiza ambayo ni tamthilia Talaaka itakayokuwa ikizungumzia masuala ya ndoa na talaka na kupeleka ujumbe kwanini kunakuwa na talaka. Pia kutakuwa na kipindi cha mapishi cha Jikoni na Marion. Kwenye kipindi hiki tutawaona masupastaa wa Tanzania wakipika chakula huku wakizungumzia mambo yao.

MAISHA MAGIC BONGO kutakuwa na sinema za Kiswahili kama Nusra iliyochezwa na Ashura Iddy, Ammar Ruweth, Riyama Ally na Zuberi Mohammed. Pia kutakuwa na sinema ya Hard Price iliyochezwa na akina Sabrina Tamim na Jacqueline Wolper .

Ikiwa imebaki mwezi mzima kabla ya MAISHA MAGIC BONGO kuingia katika runinga za watanzania kwa sasa angalia kipindi gani kipo hewani ukipendacho kupitia www.dstv.com.
D3A_5080
Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic, Margaret Mathore akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

No comments: