Tangazo

September 26, 2015

Mtoto aliyepotea na house-girl apatikana Mwanza


Taarifa mpya kutoka kwa familia ya Jullu inasema kuwa mtoto wao Loveness Coletha aliyepotea na yaya wake amepatikana na mzazi wake amesafiri kwenda jijini Mwanza kumchukua.

Tunashukuru wote waliojumuika kuifariji familia kwa maneno ya kutia moyo, walioguswa na kuombea matumaini kwa sala, wote waliosambaza ujumbe kwa njia mbalimbali na zaidi sana, kwa watendaji wote wa mamlaka husika waliofanya kazi yao katika kufanikisha hili.

Asanteni!


No comments: