Tangazo

September 2, 2015

Serikali yasema hakuna deni halali la walimu ambalo halijalipwa

Na Magreth Kinabo - Maelezo

Serikali imesema kwamba imeshalipa madeni ya walimu  ya kiasi cha Sh. bilioni 5.7 ambayo yaligungulika kihalali kati ya Sh. bilioni 19.6 zilizokuwa zinadaiwa kudaiwa, hivyo  kwa  sasa hakuna malalamiko mwalimu ambaye hajalipwa.

Aidha Serikali imependekeza kwamba   halimashauri  zilizowasilisha  madeni ambayo si   halali, yenye shaka, au watumishi wasio na madai, madai ya watumishi wasio na madai, madai ya watumishi waliokwishalipwa na waliowasilisha madai ya mishahara kama madai yasiyo ya mishahara wawajibishwe.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya  Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (pichani), wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt.  Likwelile  alisema hayo wakati akitoa taarifa  ya  uhakiki wa madeni ya  walimu wa shule za msingi, sekondari na  Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya  Ufundi Stadi.

 Alisema awali wizara yake ilipokea madai ya walimu kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) na watumishi wa  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya  Ufundi Stadi(WEMU)yenye jumla ya Sh. bilioni 19.6 ikiwa  Sh. bilioni 17.4 kutoka TAMISEMI  na Sh. bilioni  2.1 kutoka WEMU.

“Madeni ambayo  hajalipwa  ni kwa sababu hakuna kielelezo juu ya madai hayo,” alisema Dkt. Likwelile .

Aliongeza kwamba wizara  yake kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali, ilifanya uchambuzi wa awali kwa lengo la kujiridhisha na takwimu zilizowasilishwa na TAMISEMI  kwa kila halimashauri  na kwa watumishi wa WEMU, ambao umeonesha kuwa na shaka na baadhi ya madai.

“Baada ya uchambuzi wa awali idara iliandaa hadidu za rejea kwa lengo la kufanya uhakiki wa madai yaliyowasilishwa. Uhakiki huo ulifanywa na wakaguzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na timu ya wakaguzi wa ndani chini ya usimamizi wa idara hiyo.

“Matokeo ya uchambuzi wa awali yalipelekea madai ya walimu na watumishi yasiyo ya mishahara kupungua kutoka Sh. 19.6 hadi kufikia Sh. bilioni 16.2.,” alisema.

 Alifafanua kwamba madai hayo yaliyohakikiwa yalihusisha walimu 16,315 kutoka halimashauri 147 na watumishi, 1,152 kutoka WEMU. Madai yasiyohakikiwa ni Sh. bilioni 3.3 yakihusisha walimu 1,448 ambao hawakuwa na cheki namba na walimu 1,834 ambao cheki namba hazikuonekana kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya utumishi wa Serikali.

Dkt.Likwelile alisema kazi ya uhakiki katika halimashauri na WEMU ilifanyika kuanzia Machi 12, mwaka huu hadi Aprili 11, mwaka  huu.

 Aliongeza kwamba matokeo ya uhakiki yameonesha kiasi cha Sh. 5.7 kimekubaliwa na kiasi kilichokataliwa ni Sh.bilioni 10.5.

“Zoezi hili la uhakiki wa madai limeiwezeshha Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na iwapo malipo yangefanyika  bila kufanya  uhakiki,” alisisitiza.

 Alizitaja  baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni kuendelea kuwepo kwa madi ya muda mrefu kwenye halimashauri , baadhi ya madai kuwasilishwa kama  madai ya mshahara, kutokuwepo kwa kumbukumbu za madai kwenye majalada ya watumishi, majalada ya walimu kutopatikana na hivyo baadhi ya madai kutohakikiwa.

Changamoto nyingine ni baadhi ya madai yaliyokwisha kulipwa kuwasilishwa kama madai mapya na baadhi ya madai kuwasilishwa zaidi ya mara moja kwa madai yanayofanana. Akitolea mfano wa madai hayo  Mkaguzi wa mifumo ya kompyuta kutoka wizra hiyo alisema  yupo mwalimu aliyekuwa akidai  Sh. milioni 500, wakati deni  sahihi ni Sh. laki tano.

No comments: