Tangazo

October 29, 2015

DK. MAGUFULI NDIYE RAIS WA AWAMU YA TANO TANZANIA ASHINDA KWA ASILIMIA 58.46

TUME ya taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imemtangaza Ndugu John Pombe Magufuli (Dkt) Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM kuwa Mshindi wa kiti cha Urais kwa kupata kura 8,082,935 sawa na 58.46% na kumshinda Mpinzani wake ndugu Edward Ngoyae Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura 6,072,848 sawa na 39.97%. 

 Wagombea wengine na vyama vyao ni:-

Anna Elisha Mgwira (ACT Wazalendo) kura 98,763 sawa na 0.65%
Chief Lutalosa Yemba (ADC) kura 66,049 sawa na 0.43%
Hashim Rungwe Spunda (Chauma) kura 49,256 sawa na 0.32%
Kasambala Janken Malik (NRA) kura 8,028 sawa na 0.05%
Lymo Macmillan Elifatio (TLP)8,158 sawa na 0.05%
Dovutwa Fahim Nasoro (UPDP) kura 7,785 sawa na 0.05%


Akitangaza Matokeo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva.

Dondoo muhimu:
Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 23,161,440.
Waliojitokeza kupiga kura ni 15,589,636 sawa na 67.31%
Kura halali zilizopigwa ni 15,193,862 sawa na 97.46%
Kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na 2.58%.

No comments: