Tangazo

November 12, 2015

Mshindi wa Airtel Trace Nalimi Mayunga kukutana na Akon Marekani

Nalimi Mayunga akiimba katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika

xxxxxxxxxxxxxxxxxx

- Aenda kupata mafunzo  pamoja na kurekodi wimbo na video  na mwanamuziki nguli Akon

DAR ES SALAAM

MSHINDI wa shindano la musiki la Airtel Trace Music Stars Afrika Nalimi Mayunga  anatarajiwa kuondoka nchini jumatatu ya tarehe 16 Novemba kwenda Marekani  kwaajili ya mafunzo na kurekodi single yake
na mwanamuziki Nguli  Akon.

Malimi Mayunga aliibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Afrika katika mashindano yaliyoshirikisha nchi 13 barani  Afrika yaliyofanyika nchini Kenya mwanzoni mwa mwaka huu na kujishindia zawadi nono ikiwemo
deal ya kurekodi wimbo  na video pamoja na kupata mafunzo ya mzIki kutoka kwa mwana muziki Akon nchini marekani.

Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa Airtel Bwana Jane Matinde alisema"  Tunajisikia furaha kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata fulsa na kufikia ndoto zao kupitia program zetu mbalimbali
ikiwemo hii ya Airtel Trace Music Stars,  tunajivumia kumuwezesha Mayunga na kumpatai fulsa ya kujinoa kimuziki lakini pia kutanganza nchi yetu na muziki wetu ulimwenguni.

Ni matumaini yetu kuwa , program hii itamuwezesha mayunga na vijana wengine watakao pata nafasi ya kushiriki kubadilisha maisha yao na kuwa wanamuziki bora ndani na nje ya nchi na kuweza kutumia vipaji vyao kama mtaji katika kuendesha maisha yao na famila zao kwa ujumla.

 Kwa upande wake Nalimi Mayunga aliwashukuru Airtel kwa kumpatia nafasi hii ya pekee na kuhaidi kutumia fulsa hii vyema "kwangu huu ni muujiza wa pekee kupata nafasi ya kurekodi wimbo na kupata mafunzo toka kwa Akon, nawashukuru sana Airtel kwani mimi binafsi nisingeweza kuonana na Akon lakini kwa kupitia program hii na ushindi nilioupata sasa naondoka kwenda kunolewa na kupata ujuzi toka kwa Akon.

Natoa wito kwa vijana wenzangu kutokata tamaa katika kufikia ndoto zao  na kushirikia katika mashindano kama haya pindi yanapotangazwa kwani nao wanaweza kupata nafasi kama mimi leo.

Nimejiandaa vyema kuwakilisha nchi yangu na kurekodi single yangu na Akon hivyo naomba watanzania waendelee kuniunga mkono ili niweze kuwa mwanamuziki nyota duniani.


Kufuatia ushindi huo Airtel na Trace imesamwezesha  mayunga kurekodi single yake nchi South Afrika ijulikanayo kama " nice couple" nyimbo hii inapatikana  youtube na pia inapigwa katika  vyombo mbalimbali vya
habari.

No comments: