Tangazo

December 29, 2015

NAPE KUZINDUA FILAMU YA HOMECOMING UKUMBI WA CENTURY CINEMA LEO

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo anazindua filamu ya Homecoming katika Ukumbi wa Century Cinema uliopo Mlimani City.
Mwongozaji wa filamu hiyo, Seko Shamte 
Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Daniel Kijo
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo anazindua filamu ya Homecoming katika Ukumbi wa Century Cinema uliopo Mlimani City.

Uzinduzi huo pia utaoneshwa moja kwa moja na king’amuzi cha Azam kupitia Channel yake ya Sinema Zetu.

Akizungumza kuhusiana na filamu hiyo mwogozaji wake Seko Shamte alisema kuwa filamu hiyo inahusiana na masuala ya rushwa na  imekuja wakati mwafaka ambapo jami imezinduka na kupambana na janga hilo.

Alisema kuwa kwa sasa ni uzinduzi tu na kisha itaanza kuoneshwa kwa kulipia katika kumbi za Cinema kuanzia Januari 29 mwakani.

Alisema kuwa wapenzi wa filamu wanaweza kufuatilia uzinduzi huo katika chanel ya Sinema Zetu ya King’amuzi cha Azam na kuongeza kuwa ni filamu ambayo inasisimua kuangalia.

“ Hii filamu imeidhinishwa na bodi ya Filamu nchini na kupewa alama nzuri tu zinazoiwezesha kuoneshwa kwenye kumbi za sinema na hata kutumiwa na shule kama sehemu ya somo,” alisema Seko.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Azam Media, Maryam Elhaj alisema kuwa King'amuzi cha Azam kupitia Chanel yake ya Sinema Zetu kimeamua kuonesha uzinduzi huo live ili kuwapa fursa wapenzi wa filamu kuburudika zaidi.

"Najua king'amuzi cha Azam ni king'amuzi ambacho kimenuia kuwaendeleza wasanii na sanaa kwa ujumla sasa kama filamu nzuri kama hii ya Homecoming yenye viwango vya kimataifa imetuvutia na kuamua kuipa support ya kuionesha moja kwa moja uzinduzi wake na wapenzi wa filamu nao wanapata wasaa wa kuona shamrashamra ya uzinduzi wake," alisema Maryam.

Kwa upande wake mwigizaji mkuu wa filamu hiyo Daniel Kijo alisema kuwa ana imani kuwa nafasi yake ya uhusika kama kijana alieathiriwa na rushwa inatoa fundisho kwa vijana wengine wengi.

Filamu hiyo imehusisha waigizaji wengi wakubwa wa ndani na nje na kuandaliwa na kampuni ya Alkamest Media ambayo inahusika na utayarishaji wa filamu na vipindi vya runinga.

Wengine katika filamu hiyo ni Susan Lewis maarufu kama Natasha, Uncle Mshindi, maarufu kama Hashim Kambi pamoja na Abby Plaatjes aliyewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Afrika.

Pia wapo akina Isa Mbura, Magdalena Munisi, Godliver Gordian na  Michael Kauffmann na itaanza kuoneshwa kwenye kumbi za sinema kabla ya kuingia rasmi sokoni. Zaidi tembelea www.homecomingtz.com

No comments: